
LOML | Love Of My Life (50)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:50
Asubuhi niliamshwa na simu ya mama yake. Nilipoona niliogopa nilihisi Labda kuna kitu kibaya kinatokea. Nilipokea na kusema βmama shikamoo!!β
Huyu mama hakujibu hii salamu na badala yake aliniuliza βmwanangu kwema?β
Nikamjibu kwa haraka βkwema mama yangu, vipi ninyi huko?β
Huyu mama alisikitika na kusema βkwema ndiyo kila mtu analala chumba chake kweli?β
Nilishtuka, mke wangu anawezaje kusema vitu Kama hivi kwa mama yake tena. Jambo lenyewe ni dogo na kosa ni lake yeye mwenyewe.
Nilijiumauma na kusema βmama sio hivyo, ni kitu kidogo tu mama. Hata hivyo nilijisahau kumfuata haikuwa inatakiwa kuwa hivyo.β
Mama huyu alisema kwa upole βmwanangu najua ninyi ni vijana mnatakiwa kupendana zaidi kushinda sisi wazee. Sasa inakuaje wazee tunawashinda eeneh.
Ndoa yenu ndiyo kwanza mpya, mnatakiwa kufurahia, kuoneshana kila aina ya raha ya ndoa na badala yake ninyi mnagombana. Tafadhali mwanangu msifike huko.
Wewe unaishi vipi na mwanamke siku zote hizo humgusi eenh Kijana wangu. Sijui mmekoseana wapi lakini kwenye ndoa hatuweki mambo moyoni hata mkoseane nini kitanda ndiyo hakimu usimnyime mwenzako haki yake hata kama umenuna vingine havipaswi kununa endeleeni mnuno baadaye.
Sasa wewe kweli siku zote hizo anasema mwenzako unataka akafanye wapi unamtuma kufanya nini mwenzako. Jambo lingine mwanangu, jambo muhimu kwa mwanaume, kwa mwanamke kwenye ndoa na hata mwenzako nimemwambia ukitaka baraka kazini kwako, kwenye maisha yako hakikisha mkeo/mumeo ana furaha na amani na wewe.
Unapo mpa mwenzako furaha na moyo wake wa kukutakia heri unafunguka na baraka za mke/mume ni za kweli kabisa. Lakini unapo muudhi moyo wake unafunga. Mwanangu nakuomba sana. Zungumza na mwenzio myamalize analia sana.β