
LOML | Love Of My Life (51)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:51
Nilishusha pumzi na kusema βnisamehe sana mama, nimekuelewa vizuri halitajirudia.β
Mama aliendelea kusema βukiwa na tatizo lolote mwanangu niambie mama yake. Pengine kuna mambo Kama mzazi sijamfundisha mwanangu na ana kosea nitajitahidi sana ili mradi ndoa yenu iwe ndoa nzuri. Tunawaombea.β
Nilijikuta tu najibu βAmina mama, nimekuelewa nisamehe tumekusumbua.β
BaΕΔ± mama mkwe aliniaga kwa upendo sana. Na Kisha nilikata simu na kujikuta nasema βGabriella!!, Gabriella!!, Gabriella!!!β
Binafsi kuna mambo nimejifunza kwenye maisha yangu. Unajua sio kila changamoto kwenye ndoa ni ya kupeleka kwa wazazi. Kuna namna familia zetu zinachulia mambo. Mfano ninyi mnaweza kuona dogo wao likapasua mioyo Yao.
Na sio kila ukikosewa unasema nyumbani kwenu. Sisemi usiseme kuna muda mambo yanakaba unaweza kusema ili upate msaada ukiona unaelemewa na hakuna watu wanakusaidia unaweza kusema nyumbani kwenu.
Lakini hasara za kusema nyumbani kwenu ni kuwa ninyi mnapendana na ukisema kuhusu mwenzako familia inaumia na inatengeneza chuki kwa mwenzako. Kesho nyie mtapendana lakini kwa familia watamuona kama kichomi kwa binti yao au kijana wao.
Nadhani sasa unanielewa. Na kuna familia sasa unasema kijana wenu ananifanya hivi na vile au binti yenu yupo hivi na vile badala wasimame na wewe tena ndiyo unakuwa mbaya hapa sasa unajikuta unateseka na huna pakutatua matatizo yako.
Sema upande wako kama unaona kabisa unazama lakini zaidi ni ngumu sana upande wako kuona unateseka hivyo lazΔ±ma itakuwa mbaya hii. Lakini huna namna. Sasa upande wangu naumia amewezaje kusema kuwa simgusi tena kwao haloooo, alinimaliza nguvu.