
LOML | Love Of My Life (52)


𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:53
Nilimtazama vile analia, nilisikia uchungu. Niligundua mke wangu ananihitaji zaidi na mimi ninamsukumia mbali.
Sijui sana biblia lakini siku hii nilijitahidi hata nilimwambia “mke wangu najua unanihitaji zaidi. Na mimi nikaacha hasira, wivu na chuki viniendeshe. Hongera sana kwa kuwa wewe ni shujaa ukaachana na hayo maisha ya kutisha.
Ni kweli pengine umefanya vingi vibaya na huyo mwanaume lakini sasa upo hapa. İpi hapa na mimi, Rodrick. Niruhusu nikupende vile ninavyoweza na upokee upendo wangu. Hatupo kamili lakini tukingunisha huu udhaifu tutakuwa kitu kamili na kizuri sana kwenye maisha yetu.
Tujaribu pamoja kwaajili ya mtoto wetu, mtoto ana tuhitaji sana. Mke wangu Gabriella sikumbuki vizuri sana ila kwenye Isaya 43:18 Biblia inasema Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani.
Tazameni, mimi ninafanya kitu kipya. Kinafanyika sasa hivi, nanyi mtaweza kukiona. Nitafanya njia nyikani, na kububujisha mito jangwani.
Mke wangu yaliyo pita yamepita, tujitahidi kutengeneza hadithi yetu, hadithi mpya, kati yetu, mimi na wewe, sisi wawili. Upo tayari kuanza upya na mimi mke wangu na kuwa mke ambaye mimi ninatamani uwe?”
Gabriella alilia akisema “nipo tayari mume wangu, nipo tayari nakupenda sana, nakupenda mume wangu.”
Nilimkumbatia kwa furaha sana, na yeye alinikumbatia analia na mimi nilikuwa hapa namfuta machozi huku nikisema “sasa kesho jiandae nakupeleka hospitali.”