LOML | Love Of My Life (56)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:56
Siku iliyofuata niliamka vizuri na mke wangu. Na kwasababu ya Hali yake ya ujauzito nilimwambia ajiandae twende hospitali akaanze clinic yake na Kama kuna lolote lile basi daktari akatupe ushauri.

Ninakumbuka sana namna mke wangu alifurahia mimi tena ndiyo nampeleka hospitali. Nakumbuka tulijiandaa, tulipendeza sana hata mama Babuu alipotuona alisema β€œhongereni wanangu mmependeza sana.”

Gabriella wangu sasa, alijilaza mwilini mwangu akisema β€œAsante sana mama wa mimi. Haya sasa sisi tunatoka ubaki salama. Leo nina furaha niambie unataka nini?”

Mama Babuu alicheka huku mimi nikisema β€œongea na tajiri kabla hajabadilisha mawazo yake ooh!!”

Tulicheka na mama Babuu alisema β€œmwanangu unanijua ninachopenda niletee tu we unajua.”

Başı tulitoka Tuna raha. Haki ya Mungu nilikuwa simpendi mke wangu awe mke wangu. Lakini kadri najiweka karibu naye naona kabisa ninaweza kumpenda na ninaweza kuwa mwenye furaha.Tulikuwa na furaha sana na hata nilikuwa nina hofia sana kuhusu suala la mimba na kile kitu kimetokea. Ingawa hofu yangu sikuiweka wazi.

Başı tuliondoka na mke wangu ukimuona sasa alivyo na simu anachukua video, Mara anishike vindevu kidogo, Mara anibusu na nyimbo za hapa na pale. Mke wangu ana hekaheka sana za mapenzi kusema kweli. Mimi sasa ni mshamba sijui ila ndiyo mke wangu alivyo inabidi tu nizoee.

Başı tulifika kwa dokta na alikuwa ni mtu nafahamiana naye. Başı Baada ya kufika alinipokea vizuri na nikamuelezea mke wangu ni mjamzito. Akafurahi sana na alinipatia hongera sana. Baada ya hapo alimfanyia vipimo mke wangu vya afya.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UTAMU WA JAMILA FULL

JOGGING MASTER FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL