
LOML | Love Of My Life (59)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:59
Alinibusu na kwa kushikana mikono tulielekea gari na safari ilianza. Tulipita madukani kidogo kΔ±sha alinunua alichotaka nami nikamwambia nampeleka kwa rafiki yangu.
Alifurahia na vile anapenda kujulikana ni Mrs Rodricky ndiyo basi tena. Na safari ilikuwa ni nyumbani kwa Willy.Tulifika tulikuta Willy na mke wake wanafua.
Nilitabasamu, nilifurahi kuwaona namna ile.
Nilisimamisha gari na kumfungulia mke wangu mlango. Akashuka. Walifurahi sana kutuona na Willy alisema βaanh kaka suprise gani tena hizi si ungesema tu.β
Mimi Nilicheka, mke wake na yeye alimkaribisha mke wangu ile furaha unaona wazi. Lakini Baada ya muda niliona mke wangu na mke wa Willy wanaingia ndani. Willy alinitazama na kusema βwewe mjinga una bonge La mke cheki Toto.β
Nilicheka na kusema βwako umemuona bro, bonge La kitu.β
Hadithi za wanaume tena unajua, Willy tunaenda kukaa huku ananiuliza βmnaendeleaje naona mna furaha.β
Nilitabasamu na kusema βAsante kWa ushauri wako kaka. Naona ninaweza. Nimekubali ni mke wangu ni mzuri hivyo ingawa nasukumwa sana moyoni kumfuatilia naona kuna vitu sielewi lakini huu sio muda wa kuzungumza si unajua tena mazingira.β
Na kweli wakawa wanatoka sisi tunacheka tu. BaΕΔ± mke wangu aliketi mke wa Willy yeye akasema anaingia ndani. Tuliongea hili na lile pale muda wote mke wangu na simu. Sikutaka Mzuia nikawa tu nacheka. Ulipita muda Willy na yeye akaingia ndani.
Nilimtazama mke wangu alitabasamu na kusema βni pazuri, rafiki yako ni mcheshi na anampenda san amke wake.β
Nilitabasamu na kusema βsana si unaona walikuwa wanafua wenyewe.β