LOML | Love Of My Life (62)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:62
Na kuna siku akijisikia vibaya basi nikitingwa anaenda mwenyewe maisha tu mazuri sana. Mke wangu najitahidi namtoa out, amebadilika hata kama hajui kazΔ± naona ile upendo upo na anajitahidi kunijali na kunipenda hapa ndiyo anavyo jisifia ana mume mzuri, kunipamba kwa watu yupo vizuri.

Tunaenda kwao kusalimia wazazi wanafurahia, tunaenda na kwetu familia tu Zina mahusiano safi kabisa na nafurahia kuona hili kwa mke wangu huku ndani ya moyo nawaza mke wangu akijifungua salama nimpe zawadi ya gari ya ndoto zake ambalo hΓΌsema Mara kwa mara, kifupi nina furaha, lakini kuna jambo la ajabu hapa.

Simu ya mke wangu, simu ya mke wangu haikai ovyo, muda wote ana kumbatia simu yake, au yupo na simu yake. Utamuona kitandani na simu, jikoni na simu, ukiwa na yeye na simu akikaa mwenyewe na simu kuna muda mpaka chooni anaenda na simu yake.

Simu ya mke wangu ni adΔ±mΔ± sana, ukishinda naye nyumbani kuona simu yake sio rahisi.Na akiwa na simu utaona ana furaha sana anacheka ukimuuliza utasikia Giana huyu ni rafiki yake mkubwa anajua namuamini sana hivyo anajua wazi mimi sitasema kitu zaidi nasema β€œnyie Tena hapo umbea tu.”

Başı anacheka sana. Lakini ndani yangu huu ulikuwa moto, na dawa ya huu moto ilikuwa ni kuuzima na Mimi nauzima vipi sina hata maji. Ilibidi nianze kumfuatilia mke wangu bila yeye kujua kwenye suala la matumizi ya simu yake.

Başı kila nikiwa naye kitandani najifanya nimelala kumbe natazama anavyo fungua simu yake, au nikiwa naye ndani ya gari nafuatilia hilo tu mpaka nilikuja kujua namba zake za kufungulia simu. Siwezi kusahau ni 258987.Hata niamshwe nikiwa kwenye koma, kamwe siwezi sahau hii namba ya kufungulia simu ya mke wangu 258987.

Baada ya kuijua hii başı nilikuwa nashika simu ya mke wangu usiku, nikitaka kufungua roho yangu inakataa kabisa narudisha. Roho yangu inaniambia β€œkwanini umfuatilie na umeshamuoa kwanini, kwanini ufanye hivyo.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIBOKO YANGU FULL

SHEM MI NATAKA FULL

LOML | Love Of My Life FULL