LOML | Love Of My Life (72)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:72
Ukimuona ni mwanamke mzuri sana, hana shida na pesa, ni Kama vile mtakatifu, ni Kama ananipenda sana, kΔ±la Musa mume wangu, mume wangu, mume wangu Kumbe ni mchawi wa kuwanga mchana kweupe.

Kwanini anafanya hivi, kwanini hatosheki, kwanini anashindwa hata kuniheshimu mimi, kwaniniiiiiii!!!, eenh Mungu wangu, Naumia mimi, nateseka sana Pina, nateseka.”

Nilijikuta ninalia kama mtoto mdogo mbele ya Pina. Sijawahi kuongea na mtu huyu, simjui, nimewahi kumuona tu hapa kanisani lakini ndiyo nimejisikia kuongea naye haya yanayonisumbua moyo wangu.

Kusema kweli nililia sana, wakati nalia alikuwa kimya tu amefumba macho yake na yeye anatokwa na machozi. Nilikuwa ninamtazama na kutulia machozi yakinitoka tu. Halafu niliita kwa upole β€œPina!!!”

Pina alitabasamu na kusema β€œUmepata nafasi ya kulia, lia Ricky, lia mpaka ujione hautalia tena. Wapo watu wana maumivu, wapo watu wanateseka, wapo wanao pitia magumu, magumu hata kuliko wewe.

Lakini kitu kibaya zaidi ni kuwa wana rundo La maumivu kifuani, ndani yao hawapati nafasi ya kulia. Na kila akitaka kulia machozi yana goma kwasababu anakuwa anatakiwa ainuke hapo apambanie jambo la msingi ili tu yeye kesho aamke tena akilia tu anapoteza muda.

Kichwani mambo mengi sana anashindwa hata kulia. Kwahiyo wewe una bahati, una bahati sana unaweza kulia na kushusha kwa kiasi mzigo wa maumivu ndani ya kifua chako. Nakuelewa sana, nakuelewa.”

Nilimtazama machozi yananitoka, maskini huyu mrembo wangu kipofu alinikumbatia tena kwa upendo na Mikono yote miwili, alinishika kwa upendo na kunilaza kwenye kifua chake.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata