LOML | Love Of My Life (76)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:76
Nilitabasamu na kusema “nitatamani kuisikia.”
Alitabasamu na kusema “hapana, sio rahisi.”

Nilijikuta natabasamu na kusema “hata mimi natoka mbali kuja hapa na hata mimi sijui kwanini.”
Tukacheka tu, kisha niliendelea “Kwahiyo sehemu gani?
Alitabasamu akinielezea hiyo sehemu halafu akasema “ukifika hiyo kona ndani kidogo huko kunaitwa Nigeria.”

Nilishangaa na kusema “Nigeria?”
Alicheka na kusema “eenh kuna uchawi huko.”
Nikajikuta nacheka nikisema “unajua una masihara sana.”

Akacheka tena kidogo na kusema “kuna hiyo dada sasa, Ana mume wake. Lakini huyo dada mwingi sana wa habari başı mume wake huwa anapata maneno kuhusu mke wake. Akienda kumuuliza mke wake anabisha si unajua mapenzi yalivyo.

Başı nakuambia mambo yakawa mengi mdada wa watu akaona ya nini mie. Si akafanya yake. Yule bwana hasikii kawa kiziwi kabisa, anamsikia mke wake tu. Wengine mkiongelesha mtakesha ila kwa mkewe anasikia vizuri kabisa, sasa hapo utashindwa kuita Nigeria?”

Nilijikuta nacheka sana, nikisema “Pina Kumbe una vituko namna hii, nimecheka sana.”
Pina akiwa ameshikilia fimbo yake alicheka akisema “mambo ya Nigeria hayo ndani ya kinondoni.”
Nilicheka sana.

Nilicheka hata nilisahau Nina huzuni. Lakini yeye tu alinyamaza kimya. Tuliendelea na safari mpaka huko kwao ni ndani ndani kiasi nawaza huwa anatoka vipi. Tulifika hapo aliponielekeza, akaniambia “nashukuru sana, bila Shaka nimefika salama.”

Nilitabasamu na kusema “sasa hapa kwenu wapi?”
Alitabasamu na kusema “nifungulie mlango.”

Nilishuka na kufungua mlango kisha niliona mtoto anamkimbilia, mtoto mdogo miaka minne au mitano hivi. Lakini ukiona mavazi ya mtoto, namna alivyo chafuka unaona kabisa wanaishi maisha magumu. Nilitamani nisaidie ila sikuwa na namna hiyo. Mtoto alikuwa na furaha akisema “mama!!, mama!!”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata