LOML | Love Of My Life (77)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:77
Walikumbatiana na alimuuliza β€œbibi yako yuko wapi?”
Mtoto alisema β€œameenda mashineni hajarudi.”
Pina alisema β€œooh amechelewa sana, haya kanisubiri nakuja.”

Mtoto alienda, nikawa natazama ile nyumba namna ilivyo sijui hata mvua ikinyesha inakuaje huku. Ni nyumba chakavu sana.

Pina alisema β€œRicky Asante kwa kunifikisha hapa. Nakuombea heri kwa maisha yako. Tafadhali nakuomba sana Ricky. Ukae mbali na mimi, kaaa mbali na mimi kwasababu sihitaji rafiki haswa mume wa mtu.”
Nilishtuka na kusema β€œPina, usinifanyie hivyo tafadhali.”

Pina alitabasamu na kusema β€œUwe na usiku mwema Ricky, Mungu atakusaidia kila kitu kitaenda sawa. Niahidi tu utazingatia niliyosema.”
Nilimtazama na kusema β€œNakuahidi lakini…”

Hakutaka hata kunijibu alianza kuondoka zake. Mimi nilibaki namtazama nikiita β€œPina!!!, Pina!!, tafadhali.”
Hakutaka hata kunisikiliza, nilijikuta napata huzuni tena ndani ya moyo wangu kwanini Pina hataki Tena kuniona, ni kwanini?

Nilijisikia vibaya sana, nikiwa nimesimama natazama vile anaenda, anamchukua mtoto wake kwa upendo wanaingia ndani. Roho inaniuma sana. Alinitazama tu sasa sijui aliniona au ni nini, maana alinigeukia Mimi nikaita tena kwa huruma β€œPina nakuomba.”

Aliingia ndani, ninakumbuka niliingia ndani ya gari Baada ya kusikia simu yangu ikiwa inaita sana. Alikuwa ni mke wangu. Simu Ina missed calls za kutosha. Nilichukia hata kuona jina pale eti wifey. Niliumia sana.

Baada ya hapo nikatoa sauti simu yangu kwanza. Sasa wakati nataka kuondoa gari tu. Niliona pale kwa Siti alikaa Pina kuna simu ndogo chakavu. Niliitazama na kusema β€œPina!!”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIAPO CHA MASIKINI FULL

UKO HOME NIJE FULL

BINTI MDUNGUAJI FULL

JOGGING MASTER FULL