LOML | Love Of My Life (80)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:80
Kinacho nifikirisha ninavyoteseka naumia, Ina maana wanawake, wake za hao jamaa wanateseka na wanaume wa hivi hata lini. Ndoa kwani ni lazima iwe hivi kuumizana mbona Willy na mke wake wanaishi kwa raha sana.

Unawezaje kuwa na watu ulio lala nao kwenye ndoa yako, hakuwaza mimi nikijua itakuaje, sio tu wao kuwepo kwenye sherehe ni Mc na msimamizi hivi sijui hata unanielewa.

Sitamani mwanamke mwingine ufanye hili kosa, sitamani mwanaume mwingine ufanye kama alivyofanya mke wangu. Baraka zinatoka wapi kwa ndoa kama hii, watu unatuficha, Mungu utaweza kumficha, kumdanganya na kufanya asione. Sio kweli. Heshimu ndoa, heshimu agano hili ili ndoa yako iwe ni ndoa yenye baraka nyingi kutoka kwa Mungu baba wa mbinguni.Ni kitu kidogo sana, kidogo mno.

Niliendesha gari, Nilifika mpaka hotel ambayo nilitaka kulala siku hii. Nilipofika nililipia na kisha kupewa chumba. Muhudumu alinisindikiza mpaka kwa chumba ambacho nilikuwa Nimepewa. Nilimshukuru na kuingia ndani ya kile chumba.

Wakati naingia ndani nilikumbuka maneno ya Pina, sauti yake ya upole na unyenyekevu akisema β€œMungu akuongoze, jiweke karibu na Mungu. Atakupa sababu kumi elfu za kuwa na furaha hata mambo yakiwa magumu zaidi jua Mungu yupo hapo kuna mahali anataka ufike. Wewe ishi tu.”

Nilitokwa na machozi, nililia sana hata nikakumbuka tena aliponiambia β€œSukari haina thamani kwenye supu, na chumvi haina thamani kwenye chai. Δ°li Supu iwe tamu inahitaji chumvi na ili chai iwe chai inahitaji sukari. Jua thamani yako, kaa unapotakiwa kukaa.”

Nililia nikapiga magoti na kusema kwa Mungu β€œUnanifahamu vizuri Mungu, ninajua ninayo mapungufu mengi sana kwako lakini najua sina kitu kibaya nilicho kutendea hata umenikutanisha na mwanamke huyu.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

SHEM MI NATAKA FULL