LOML | Love Of My Life (81)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:81
Nilikuwa tayari kumlinda, kumtetea, kumpenda na kumfanya wangu wa maisha ili kutimiza kiapo nilicho kula kanisani kwa jina lako. Lakini Mungu wangu, ni mwanamke gani huyu, yupo kinyume na wewe, yupo kinyume na jamii, yupo kinyume hata na mimi Mungu wangu ni mwanamke wa namna gani huyu.

Aninipitisha kwenye miiba, kwenye moto, kwenye vipande vya chupa na nipo peku viatu vyangu anavyo yeye. Amenikata nipande vidogovidogo kadri awezavyo. Mungu nionyeshe njia, Mungu nivushe, Mungu nisaidie, Mungu ninakutegemea, Mungu usiniangushe, Mungu Naomba hekima zako.

Ninakutegemea, ninakupenda natumaini unanisikia baba yangu, Oooh Mungu wangu, Ooh baba yangu, nisaidie Yesu, nisaidie roho mtakatifu, mimi ni mtoto wako Mungu, kamwe sijawahi kuacha kukuamini.”

Nililia sana, na vile Pina aliniambia ukipata muda wa kulia lia, lia sana maana kuna watu wanatafuta muda walau walie wanakosa muda. ukipata muda wa kulia lia haswa. Mimi hiki chumba, hii hotel, sitaweza sahau Ina machozi yangu ya kiume mengi sana, nililia kuliko kawaida. Sikumbuki mimi kama kwenye maisha yangu nimewahi kulia Kama ambavyo nilikuwa nimelia siku hii. Nilikuwa nimelia sana, nililia kuliko nilivyowahi kulia tangu nizaliwe.

Gabriella, alivyo mcheshi, mzuri, mwenye pesa, anavyo jifanya kuniita kΔ±la muda mume wangu, mume wangu, Dadie, Dadie baby nyingi Kumbe Hakuna kitu mimi ni kivuli tu, mimi sio uhalisia wa maisha yake. Mapenzi anayogawa na kupata huko nje ni makubwa kuliko ninayo mpa. Huyu mke wangu alinifungua macho sana.

Kuna watu ni wazuri, tunawapenda, ni watu wema, ni watu wamependeza na tunatamani kuwa Kama wao wakati mwingine. Kumbe watu hawa ndani Yao wameoza.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata