LOML | Love Of My Life (82)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:82
Simaanishi watu wote wameoza, ndiyo baadhi Yao wanatumia uzuri wao, umaarufu wao, na mengine mengi mazuri Kama kivuli tu cha kuficha yaliyomo ndani yao.

Pengine wasingekuwa na vitu hivyo wangekuwa chakaramu. Mke wangu huwezi mfikiria haya, hata mimi Sikutaka kumuoa sio kwasababu ya haya. Ni moyo wangu tu hakutaka awe mke wangu kabla hata sijamuona Pina.

Sikuwa namuona kama mke wangu. Na ni kitu tu sikuwa nacho wakati wa mahusiano. Aliponiambia tu ana mimba ndiyo nilianza kujihisi tofauti. Kumbe hii ilikuwa ni ishara.

Kamwe kwenye maisha yako usipuuze hisia zako juu ya kitu fulani. Na pengine sasa unapitia unacho pitia kwasababu tu ulipuuza ishara Fulani.Kumbe Mungu alikuwa anajaribu kukusemesha na kukuvusha hapo.

Mungu ana zungumza na watu wake kwa njia nyingi sana. Hisia za ndani, ndoto, maono, na hata kupitia maneno ya mtu mwingine au hadithi ya mtu fulani. Mfano umekaa unafikiria mbona sijalipa zaka, kwanza hata sio muhimu sitalipa nitalipa mwakani.

Siku utakayo waza hili unakuta unaingia mtandaoni unakutana na zaka, unaenda status unakutana na mtu kapost meme ya zaka, ukizunguka huku unakutana na zaka. Halafu bado una puuza hutoi zaka sasa unafikiria umefanya nini hapo?. Tuendelee na simulizi yetu.

Lakini kabla tupate tangazo kidogo, Simulizi hii ni simulizi ya @agathadastorywriter instagram napatikana hivyo. Ukiona popote na ukiuziwa na yeyote tofauti na mimi huyo ni mwizi. Karibu instagram na ufaurahie simulizi zangu nyingine nyingi Asante.

Nilitumia muda pale chini, kisha Baada ya kulia sana nilijikongoja na kushika simu yangu. Kusema kweli nilitamani sana niwashe ili nimpigie Pina. Lakini roho yangu ilikataa kabisa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata