
LOML | Love Of My Life (84)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:84
Mama alisema kwa ukali βsina muda wa kukusikiliza fanya haraka Njoo hospitali, na sijui utatazama vipi Wakwe zako. Mwanangu umekuaje?, mpaka mnapoteza mtoto haupo?, umeniangusha sana.β
Nilichoka, sijui nini kimetokea mpaka mimba imetoka kwa Gabriella. Mama Alikata simu hata hajanisikiliza kabisa.
Niliumia, niliumia kwasababu nimeona hakuna atakayejali mimi napitia nini mara zote wanaume ndiyo tunaonekana tuna matatizo Kumbe hapana.
Nilijikuta naumia kuona mama yangu hanisikilizi tena, hana hata muda wa kujua nimepatwa na nini.
Mimba ya Gabriella iliniuma sana. Ni kweli nimegundua sio yangu, kupitia meseji na sijui Kama aliyeambiwa pia ni yake kutokana na tabia za mke wangu. Lakini Mungu peke yake ndiyo anajua, mpaka nilimuoa ni kwasababu sikutaka kukataa mimba, sikutaka kulea mwanangu kihuni, nilitaka kuwa baba, nililea na kutunza mimba hii.
Roho yangu inauma zile hekaheka. Kumpa kΔ±la anachotaka kuanzia chakula hata nilikuwa naandaa wakati mwingine Kumbe najitesa bure. Mtoto hana hatia, kama sehemu ya maisha ya mtoto huyu niliumia lakini mbele ya Mungu, yaani ardhi na mbingu.
Sikuwa natamani kabisa kumuona Gabriella kwenye macho yangu.Sikuwa natamani. Lakini sasa nitafanya nini, natakiwa nikaonekane na ndiyo tutapata muda wa kufanya mambo mengine kuamua juu ya ndoa hii. Kitu pekee ninachowaza ni kuachana na mke wangu kΔ±la mtu aishi maisha aliyochagua.
Nilitoka pale, nilijikaza haswa. Nilifuta machozi yangu kiume. Niliweka mambo sawa hapa Hotel na kuondoka zangu. Niliendesha gari nikiwa nawaza mambo mengi sana. Nilikuwa nina mawazo kusema kweli.