
LOML | Love Of My Life (86)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:86
Mama huyu alilia akisema βmume wangu, uliona hali ya mwanangu lakini.β
Huyu baba alimtoa mke wake nikabaki nimechoka, na wakati huo mama yangu na baba na wao walinifikia. Mama alinitazama na kusema βUmeona sasa mwanangu eenh, kwanini tugambane sisi ni familia.β
Nilipoinua uso wangu, nilisema tu βmama nimechoka sana, mnaniumiza sana na maneno yenu. Hakuna anayejali kuhusu mimi, nimelala wapi, nimetokewa na nini, wote mnanilaumu tu. Hii ndiyo namna ya kuwa mzazi?, mtu wa karibu, au mtu anayejali familia yake?. β
Baba alinitazama akanyoosha kidole na kusema βmwanangu upo sawa kweli?, macho, macho, macho yako, uso umee, umee..β
Nilijikuta kwa uchungu nalia nikisema βbabaaa!!, baaaaabaaaaa!!, baba!!β
Baba yangu alinikumbatia, alinikumbatia kwa uchungu kisha aliniambia βTulia mwanangu, wewe ni Simba wangu, jasiri, mtetezi na rafiki yangu. Acha kulia tafadhali. Nakuomba.β
Mama niliona akishusha hasira akisema βmwanangu kuna nini mbona unanichanganya.β
Baba alisema kwa upole βmke wangu, kaendelee na mgonjwa mimi natoka nje na kijana wangu. Nahitaji kuzungumza naye.β
Mama alinitazama na kusema βpole mwanangu, nisamehe sana.β
Nilimtazama tu lakini kuna jambo nilipata kupitia haya mambo.
Wazazi wetu wengi hawajui tabia za watoto wao. Wazazi muda wote wapo kwaajili tu ya kutetea mtoto. Na pengine tabia hizi kuanzia mtoto anakua nazo lakini wewe umekaa kuangalia mazuri na vile unajua kulea basi unaona umemaliza.
Watoto hujifunza mengi kwa watoto wenzake, majirani, jamii, na huko shuleni. Mzazi peke yako hautoshi. Ukisikia jambo kuhusu mtoto wako awe amefanya au hajafanya jitahidi ufuatilie na usiishie hapo tu tafuta namna nzuri ya kumkanya na kumfundisha ili awe mtoto mzuri kwa wengine na kwaajili ya kesho yake.