
LOML | Love Of My Life (87)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:87
Wazazi wengi ukimpa changamoto za mtoto anakua mkali, anakuona mchawi wa maisha yake na usikute ni kweli mtoto ana haribika. Kumbuka ni mtoto wako akiwa tumboni, Ni mtoto wako akipata matatizo.
Lakini mtoto wa wote akiwa amezaliwa na yupo sawa hana tatizo lolote huyo ni wa wote yaani jamii nzima. Tazama wazazi wa mke wangu, hawawazi hata mtoto wao pengine kanikosea mimi, au nimepata matatizo mimi. Wote wanafikiri mimi ndiyo mkorofi kitu ambacho kimezidi kuniuma roho yangu. Nimeumia zaidi.
Mimi na baba yangu tulianza kutoka, wakati tunatoka nilikutana na Giana na mama babuu. Giana aliponiona tu aliuliza βshem salama kweli?β
Ndiyo mtu wa kwanza hapa kuona sio sawa kwangu. Nilikumbatiana naye na kusema βshem, tutazungumza nataka kuongea na baba kwanza.β
Alinitazama tu, kisha aliniambia kwa upole βsawa napeleka chakula, tutaongea shemeji yangu. Be strong super shem please.β
Kinyonge nilitabasamu.
BaΕΔ± nilitoka na baba yangu na tulipata mahali tulikaa. Baba alinitazama na kuniambia βkΔ±jana wangu, ni wazi kuna kitu kimetokea. Tafadhali, kuwa muwazi mimi ni baba yako. Tunacho zungumza hapa nakuomba kitakuwa baina yetu kama hutaki mama yako ajue. Nataka kukusaidia hata mawazo tu.β
Nilitabasamu huku machozi yakΔ±nΔ±toka. halafu nilifumba macho yangu na kusema βbaba, jana nimegundua kitu kibaya sana. Mke wangu ana mahusiano na mwanaume mwingine tena ninaye mfahamu na ndiye aliyekuwa baba wa mtoto.β
Baba yangu alishika kichwa chake na kusema βOooh, noooo!!, nooo!!, why!, kwanini linatokea hili, nini hiki Mungu!!β
Nilijikuta nalia nasema βnaumia baba, nateseka, naumia.β