
LOML | Love Of My Life (90)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:90
Alishangaa na kuniuliza βuna maana gani shem, mbona sijui kitu amefanya nini tena?β
Nilimwambia kwa kukasirika βGiana nakuamini sana, naona una heshima, una hofu ya Mungu, unaweza kumuongoza mwenzako sitaki kuamini wewe uwe mwanamke mwema halafu mwenzako awe na tabia mpaka shetani anakaa pembeni anashangaa huyu kiumbe ni mali ya nani maana kwake hayupo kwa Mungu hayupo.
Natamani niongee maneno mabaya zaidi lakini unajua nini?, nakuheshimu sana. Kama ni tabia zenu mbadilike, kama ni Gabriella ndiyo ana ushenzi ule basi haufai kuwa rafiki yake.
Kwasababu rafiki wa kweli atamvusha mwenzie awe njia salama au na yeye aende upande mwingine. Sio kuitana dada, twin, bff, mara ndugu yangu kumbe upumbavu mtupu, Uwe na siku njema shemeji.β
Shemeji yangu alichoka, sasa pengine na yeye ni kama wazazi unajua kuna watu wapo vizuri kwa kuficha mambo yao mabaya sana. Mke wangu pengine na rafiki yake alimficha. Mimi sikujali nikawa naendelea ma safari yangu ya kurudi ndani ya hospitali nikamuone huyo mtoa roho yangu.
Wakati nimeinamisha kichwa changu nikakutana na mama babuu. Alinisimamisha na kusema βPole sana kijana wangu.β
Ni mama mstaarabu na mzuri sana huyu, ana upendo sana. Nilijikuta namkumbatia na kisha nilisema βnini kilitokea mama babuu!!, nini kimesababisha kupoteza mtoto?β
Alinitazama na kusema βnilikuwa jikoni, ghafla nikasikia mtu analia, wakati natoka alikuwa tayari ameanguka na anatokwa na damu sana. Ndiyo nikaomba msaada kwa mlinzi wa kupata gari na kisha niliwataarifu nyumbani.β
Nilivuta pumzi na kusema βpole sana mama babuu, nilipaswa kuwepo.β
Alinitazama na kusema βmwanangu, nakuhurumia sana. Naona unavyojisikia. Unajua nini boss?β