LOML | Love Of My Life (93)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:93
Gabriella alianza kulia pale, alilia wakati huo mama yake anaingia sijui alikuwa mlangoni mimi sijui ila aliingia na alikuta mwanaye analia akisema β€œMume wangu nimekukosea, najutia, nakupenda mume wangu, tafadhali usiniache, bado nakuhitaji sana. Nakuhitaji mume wangu, wewe ni kila kitu kwangu.

Mama nakuomba niombee msamaha kwa mume wangu, ananiacha mama, nitakuwa mgeni wa nani, nampenda mume wangu, nimemkosea sana naona aibu, mume wangu amefanya kila kitu kwaajili yangu tafadhali sana, nakupenda mume wangu, nisamehe mimi, nisamehe.”

Vile analia mimi nashangaa maana awali aliapa hata kwa biblia kuwa harudii kutoa kinyume kumbe ndiyo tabia yake.

Nilikuwa namtazama nashindwa zuia hisia za kucheka na kulia huku mama yake akiniuliza β€œmwanangu kuna nini, eenh mnanichanganya. Tulia Gabby, unaumwa unatakiwa kutulia. Mwanangu shida nini, eti Rodricky.”

Nilimtazama na kusema β€œmama, zungumza na binti yako, yeye anajua kila kitu. Na akitoka hapa nenda naye kwako, simuhitaji kwangu tena, simuhitaji.”

Mama aliachia mdomo, kama ni filamu basi hapa ni ile sehemu mdundo wa mshangao unapiga halafu tunashangaana, Gabby analia akisema β€œnooo hubby, mume wangu.”

Sikujali, ni kama filamu basi hapa ule mwendo wa mgandisho natoka kwa maumivu nafuta machozi ndiyo yanazidi. Hii siku ilikuwa siku ngumu sana katika maisha yangu, ngumu sana.

Nilitoka pale, mama yangu ananiita kwakweli sikuwa na hali ya kuongea na yeyote. Nilitoka mpaka nilipoweka gari yangu, nilipanda gari yangu na kuanza safari yangu ya kuelekea nyumbani. Nilimtii baba yangu, mwanaume hakimbii nyumba yake, anasimamia majukumu yake.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

CHAGUO LA MOYO FULL

BIOLOGY TEACHER FULL