LOML | Love Of My Life (95)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:95
If you disappeared because I seemed like too much, I understand. But please know, my mistakes wasn’t rejection nakupenda haki ya Mungu.

Nina ujinga mwingi lakini upendo wangu kwako ni wa kweli kutoka moyoni, sijui nini kinanitokea, niamini nateseka sana, nateseka sana mpenzi, naona aibu, hadithi yangu sio nzuriπŸ’”πŸ˜­, bahati mbaya siwezi chana kurasa hizi.

It was pain I couldn’t explainπŸ’”πŸ’”πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­. Lakini nipi hapa, mimi nipo hapa, naomba nafasi nyingine, naomba tuzungumze, naomba nikuelezee kila kitu kunihusu, shida zangu na mizigo yangu pengine utanisikia na utaniongoza kwa njia nzuri, wewe ni furaha yangu, wewe ni kitu nahitaji, wewe ni malaika wangu usiniache, nifundishe, niongoze nipo tayari kuwa mwanamke bora, uniache tu kama chombo cha starehe, mimi ni mke wako, wewe ni mume wangu. Nimekukosea nisamehe, NAKUPENDA SANA, NAKUPENDA MPENZI WANGU, nakupenda mume wangu, nihurumie nateseka haki ya MunguπŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ’”β€

Unamjua mke wangu na kizungu chake, ukikaa vibaya unamuonea huruma. Anafanya tu mambo kunivuruga mtoto wa watu. Niliposoma hapa nilimuhurumia nikaona labda kuna jambo ana pitia, lakini ni jambo gani hili ambalo linafanya awe namna hii, jambo gani linafanya awe wa wengi, hatosheki na ana maisha ya ajabu namna hii. Niliacha kwanza kumtafuta Pina.

Niliweka simu yangu pembeni, nilitazama juu tena nikiwa na maumivu na kusema β€œMungu wangu, nakushukuru sana, nakushukuru kwa mengi sana.Najua maisha sio rahisi ingawaje ninaonekana kupata vyote, wewe peke yako ndiyo unajua namna umenisitiri, umenibeba na mengi, umenivusha na mengi, umenitengeneza na kunibariki na mengi sana.

Sijui sana kuhusu haya, kwanini na una mpango gani na mimi hata nipite kwenye barabara hii. Lakini ninaamini, kwakuwa nipo hapa, ninayo pumzi na afya njema basi wewe uliyeniumba mimi, upo upande wangu, una kazi na mimi, unanitengeneza Mungu, ninakuamini.

Uvumilivu wenye utulivu, unikumbushe siku zote kuwa wewe ni baba, baba mwenye mipango mizuri na mimi, baba mwenye kunipenda na kunijali, na kunitunza. Naamini upo na mimi, sijui unataka nifanye nini, ila nitavuka.” Nilishusha pumzi na kujilaza tena

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIBOKO YANGU FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

CHAGUO LA MOYO FULL