LOML | Love Of My Life (97)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:97
π•Ύπ–Žπ–’π–šπ–‘π–Žπ–Ÿπ–Ž π•·π–Žπ–‡π–—π–†
Nilishangaa, nilishindwa kujizuia kabisa kumuuliza swali hili β€œumejuaje ni mimi?”
Alinijibu kwa upole β€œhisia na kumbukumbu zangu. Nikimsikia mtu mara moja basi hata upite muda kiasi gani, nitafanya jitihada bila kukosea nitajua tu.”

Nilitabasamu na kusema β€œsafi sana, nimefurahu.”
Pina akaniuliza β€œunataka nini Rodricky?, umepata vipi namba yangu kwasababu sikumbuki kama nilikupatia.”

Nilianza kujiumauma, aliniendelea na kusema β€œalright, ni sawa haya unataka nini?, nilishasema kuwa sihitaji unitafute tena, sihitaji.”

Nilijibu kwa upole β€œnakuomba usikate simu Pina. Nisikilize huna haja ya kuwa na hasira. Mimi sio mtu mbaya, nilitaka kukujulia hali, na kuomba kukuona tena. Naomba nikuone tena, nahitaji kuzungumza na wewe tena, nakuomba.”

Pina alinijibu bila kuficha β€œhaiwezekani, hapana Ricky, sihitaji kukuona tena, naomba kaa mbali na mimi.”
Alikata simu, niliita ili hali najua amekata simu β€œPinaaaa!!, Pinaaaaa!!!, Pinaaaa!!!”

Nilitoa simu masikioni na kusema β€œni nini tena hiki, Mungu wangu. Pina hataki kuzungumza na mimi. Ooh.”
Nilijilaza pale kitandani, nilijisikia vibaya na ndani yangu nilidhamiria lazima nitaenda kumuona tu nyumbani kwao ni lazima.

Sikutoka hata chumbani kwangu, ninakumbuka nikiwa chumbani rafiki yangu Willy alipiga simu. Aliniambia β€œkaka unakwama wapi, wale wateja wamekuja wanahitaji mzigo wa kutosha na wewe huokoti simu, nimefika mpaka kazini kwako sikupati. Hakuna anayejua taarifa zako tunafanyaje kazi namna hii kaka?”

Nilivuta pumzi na kusema β€œnisamehe sana kaka, nisamehe sana. Unajua mke wangu alipata changamoto. Mimba ikaharibika basi ndiyo imekuwa hivyo hapa bado yupo hospitali.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

TOBO LA PANYA FULL