
LOML | Love Of My Life (98)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:98
Willy alisikitika na kusema βooh jamani hii ni mbaya, mpo hospitali gani naweza kuja kuwaona baadaye.β
Nilimwambia kwa upole βusiwaze kaka, kwasasa nipo nyumbani nimechoka sana. Kesho nitakwenda tena, na pia nitajitahidi niingie kazini walau niendelee na maisha mengine.β
Willy aliniuliza βupo sawa lakini?β
Nilijikaza na kusema βnipo sawa.β
Willy alisema βnaelewa maumivu ya kupoteza mtoto, nakuelewa vizuri sana. Mtoto uliyemtarajia na ulijiandaa kwa jina jipya. Usijali kaka Mungu ataleta mtoto mwingine.β
Nilitabasamu, machozi tu maana kusema kweli hata ndoto ya kuwa na mtoto naona tu inapotea mdogo mdogo.
Niliagana na Willy na kuendelea tu kujilaza.Wakati wote huu mke wangu ni anapiga simu, anatuma text za kunibembeleza akiniita majina mazuri βbaby sorry, Dadie please, Nakupenda mume wangu.β
Mke wangu akiwa kwenye eneo la kuomba msamaha anajua kutumia nafasi vizuri kabisa.
Usingizi ulinichukua, tena sio wa kitoto. Hata nilipokuja kuamka ilikuwa ni siku mpya, siku nyingine kabisa. Nilisimama na kuchungulia dirishani. Nilitazama jua nikisema βusinisahau Mungu, kama jua linapochomoza kila asubuhi na maisha yangu yawake kama jua hili kila siku mpya inapoanza. Nikumbuke Mungu wangu.β
Nikiwa pale dirishani, tena niliendelea kuwaza. Itakuwa hivi hata lini?, ninatakiwa kwenda kazini. kurudi kazini na kuendelea na kazi ili nijichanganye. Maana ninavyokaa hivi bila kazi nawaza vitu vibaya. Nawaza kuwaumiza hawa wanaume wote ambao mimi nimewafahamu sijui kuhusu wengine.Lakini hawa ambao nimewafahamu kiukweli nawaza kuwaumiza tu.
Nilieleka bafuni, unajua sasa nimebadilika. Uso wangu hata furaha ya kulazimisha siwezi, nashindwa kabisa kulazimisha furaha. Nawezaje kulazimisha furaha ambayo ni ngumu sana kuipata kutokana na haya mambo ambayo yananitokea. Niliamua niende kazini kwanza nikapunguze mawazo.