
LOML | Love Of My Life (103)


๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:103
Nililazimisha tabasamu, alikuwa anainua mikono kunipokea, nikaenda kumkumbatia huku moyoni natamani kupasuka. Kisha aliniambia โumependeza sana mume wangu.โ
Nilitabasamu na kusema โnashukuru mke wangu.โ
Basi hawa marafiki zake, wananitazama, wanatabasamu wenyewe laiti wangejua.
Wangekimbia, basi Gabriella alinitambulisha โgirls.Huyu ni shemeji yenu, wengi mnamfahamu, so this is my Ricky, my handsome hubby, hubby hawa ni rafiki zangu nimesoma nao chuo na sasa wapo hapa nchini.โ
Niliwatazama na kusema โnimefurahi sana kuwaona.โ
Mke wangu alisema โshemeji yangu, nimefurahi kukuona.โ
Willy alisema โpole sana shemeji yangu, Mungu atakusaidia utakaa sawa.โ
Gabriella alisema โAmen shem, nitaomba Mungu asichelewe kutupa mtoto mwingine.โ
Marafiki zake waliitikia โAmen!!โ
Sasa hapo anavyo nishika, ni kama kila kitu kipo sawa. Hii siku nilikuwa nashangaa sana moyoni.
Usione watu wanapendana unawafahamu, unaona wanayofanyiana mbele yako, mbele yenu, mitandaoni ukajihisi wewe hupendwi. Wapo watu hawapendi kuonekana wameshindwa, watu wana trauma zao na kujidanganya ndiyo wanaona wanakuwa na furaha.
Kuna mtu anaweza fanyiwa tukio lakini kesho akapost na caption yenye makopa kuaminisha watu yeye ni bora. Kuna watu ndani hawalali hata chumba kimoja ila wewe ukiwaona unasema Mungu haya mapenzi na mimi yanipate.
Watu hawakutani hata kimwili, hawawasiliani ila angalia namna wanaonesha wapo sawa. Gabriella kazi anaweza, mimi kwakweli nashangaa sana.