
LOML | Love Of My Life (105)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:105
Mimi na huyu mama pamoja tulitoka. Tulipofika nje nilipitiliza mpaka kwa rafiki yangu. Nikamuelezea kuwa natakiwa kuzungumza na huyu mama kwanza. Basi rafiki yangu aliniambia βkuna mahali nawahi. Ninatamani pia kuzungumza na wewe ila sio lazima leo.β
Nilitabasamu kivivu na kusema βnakuelewa. Kwakuwa hukuja na usafiri ondoka na langu utaacha ofisini pale mimi nitajua namna ya kuja.β
Alitabasamu na kusema βhaina shida kaka asante.β
Nilitabasamu tu, rafiki yangu akawa anaondoka zake na mimi nilibaki hapa na sasa natakiwa nikaongee na mama mkwe wangu. Tunaenda kuongea nini sijui, ila natakiwa nikazungumze na yeye.
Ninakumbuka sana namna ilikuwa, tuliongozana mimi na huyu mama mpaka sehemu ya kuketi, mimi na yeye tu sisi wawili peke yetu. Ilikuwa ni sehemu tulivu sana.
Baada ya kufika mahali hapo, nilimtazama mama, na yeye alinitazama na kusema βnisamehe sana kwa usumbufu kijana wangu.β
Nilimtazama na kusema βusijali, Hakuna shida mama.β
Huyu mama aliinamisha kichwa chake na kisha alisema βmwanangu, nakukosea sana, naomba radhi kwa kΔ±la kitu sikupaswa kuwa namna nilikuwa niligharifika tu. Sikumaamnisha kitu.β
Alinifanya hata nikakumbuka Tena maneno yake, halafu Nilitabasamu Tena na kusema βhakuna shida kabisa , wala hata usijali ni sawa.β
Huyu mama alivuta pumzi yake Tena pumzi ndefu sana na kuinamisha kichwa chake. Nakumbuka sana namna ilikuwa.
Nilisikia Tena sauti ya mama mkwe wangu ambayo ilikuwa na utulivu sana. Ilikuwa inasikika vizuri sana, kwa ukaribu zaidi maana tulikuwa wawili tu, mama huyu alisema akitokwa na machozi na kufanya zungumza yake iwe ya maumivu sana βRodricky tafadhali nakuomba sana, usimuache mwanangu, usimuache binti yangu. Ninakuomba sana.
Ni ngumu mimi kusema, ni ngumu kuzungumza na wewe lakini kwa Mara ya kwanza Kama mama natakiwa kusimama kwaajili ya binti yangu.
Kusema kweli sijawahi kumuona binti yangu ana furaha tangu hapo mpaka alipokutana na wewe. Amekuwa mtu mwenye furaha sana, amekuwa akizungumza sana kuhusu wewe kitu ambacho hajawahi fanya hapo mwanzo.