LOML | Love Of My Life (107)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:107
Sioni hata sababu ya kwanini nilikuwa hivi uliniroga eenh, au mimba ulinisakazia tu. Maskini mkubwa wewe!!.Maana sikumbuki kama niliwahi kukupenda.

Haya maneno kama mke ambaye nampenda mume wangu yalikuwa yananitesa zaidi ya mateso yenyewe. Nilikuwa nalia.Nilikuwa nateseka sana kwasababu na kujipamba kwangu, na kujiweka kwangu bado mimi naonekana ni mwanamke nisiye na thamani.

Aliendelea kunikumbusha nilivyo Mara kwa Mara, aliendelea kunikumbusha namna nilivyo maskini na nisivyo na thamani nisiyejua chochote. Kitu ambacho sio kweli, mimi niliona ninacho kΔ±la kitu, lakini tu niliamua kuwa mke kwake.

Nilianza kutafuta furaha nje ya ndoa yangu, kosa langu kubwa sana hili na ninajutia sana. Nilikuwa naona hii ni njia sahihi ya mimi kupona, kujisikia furaha na kuwa mwenye furaha muda wote.

Hakika hii niliona inanisaidia sana maana hata muda wa kugombana na mume wangu sikuwa nao, sikuwa namuuliza tena maswali kwasababu nilikuwa napendwa, nadekezwa, nabembelezwa.

Nilikuwa sasa najihisi kama mwanamke. Najuta sana, sikutakiwa kutoka kutafuta furaha. Huko pengine nilitakiwa kutafuta namna nzuri ya kumalizana na mume wangu Kama alikuwa hanipendi.

Mume wangu alianza kupata wivu kama, lakini mimi sikujali kabisa hata kunijali kidogo tu nilikuwa naona ananiigizia. Niliendelea na maisha yangu. Nilianza kuleta wanaume ndani kwangu, nyumbani kwangu.

Nilikuwa nafanya kΔ±la ninachotaka na mwanaume ninaye mtaka popote pale iwe sebuleni, jikoni hata chumbani. Siku moja nikiwa chumbani na mwanaume fulani, niliona mwanangu anachungulia mlangoni.

Nilishtuka na kisha haraka nilimzuia Yule mwanaume kuendelea. Nikikumbuka nalia sana. Nilimfuata mwanangu chumbani na kukaa pembeni yake nikamuuliza kwa upendo β€œUmeona nini mwanangu?”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

TOBO LA PANYA FULL

SHEM MI NATAKA FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL