LOML | Love Of My Life (109)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:109
Alinisihi sana nimlinde mtoto wangu. Lakini sikujua ni namna Gani imemuathiri. Alianza kuishi maisha yake ya kujitenga sana.Lakini na mimi nilijitahidi kuokoa hili mwanangu asishuhudie.

Lakini bado nilikuwa wanaume wengine nikihisi namkomesha mume wangu. Ulifika muda na wakati sasa binti yangu amekua kidogo. Na mimi maisha yangu haya naona raha sana.

Eenh mwanangu shule tena niliitwa safari hii kesi ilikuwa amekutwa na mtoto mwingine wakajaribu kufanya mapenzi. Hii iliniuma zaidi, waalimu walielekeza sana Ila niliona sasa wanazidisha binti yangu hata kama hawezi kuwa hivyo bado ni mdogo sana.

Ninakumbuka tulivyotoka ile shule sikumrudisha tena. Nishindwa kufuata ushauri wa waalimu na nilifanya maamuzi kama mzazi nisiyetaka maelekezo.

Mwanangu aliendelea na maisha hata nilimtafutia msaikolojia amsaidie kiakili. Na lilikuwa linaenda sawa sana hata kufika sekondari. Niliitwa shule kuwa mwanangu ana mahusiano na mwalimu. Alikuwa kidato cha kwanza tu.

Nilipofika shule mwanangu alichapwa sana. Alikuwa ma hali mbaya. Na kila anacho ulizwa anakubali tena akiwa anaonekana hajali kabisa.

Nilikuwa nachukia sana, hata nilifoka nikisema β€œhivi wewe mtoto una shida gani, una shida nakuuliza?”

Siku hii ndiyo binti yangu aliniambia kwa hasΔ±ra β€œusiniulize mama, usiniulize maswali na una majibu. Ni wewe mama, ni wewe sababu. Ninakuchukia sana, ninakuchukia sana mama. Ni vile wewe ni mama yangu, umenilea na unanitunza vizuri.

Lakini kuhusu kΔ±la kitu wewe ndiyo wa kulaumiwa. Nakuchukia sana, nakuchukia sana, nakuchukia mama, wewe sio mama mzuri kabisa.”

Alitoka analia hata waalimu walibaki wanashangaa, nilipata aibu, kusikia mtoto wako anasema anakuchukia, ni aibu na maumivu vyote kwa pamoja, lakini nilitakiwa kumfuata, nilimshika mkono mwanangu alisema β€œNiachie mama, umeharibu maisha yangu.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UTAMU WA JAMILA FULL

CHAGUO LA MOYO FULL

JOGGING MASTER FULL

LOML | Love Of My Life FULL