
LOML | Love Of My Life (111)


𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:111
Natamani wakina mama wangejua namna ya kuishi na watu hawa, natamani wangeheshimu usiri sana wa tendo hili ili wasirudie makosa yangu. Mimi nilisababisha tatizo kısa ugomvi wangu na mume wangu.
Baada ya kuondoka hapa, nilimuacha mwanangu nyumbani na nilianza kupambana na Jimmy. Nilimfuata mpaka kwake, tuligombana sana na nilimuhakikishia nitamnyoosha na nilikuwa na nguvu hiyo kwasababu pesa haikuwa shida kumfanya chochote kile.
Sijui ilikuaje Ila jamaa alinitoroka na sikuwahi msikia tena. Na kuhusu mwanangu nikawa karibu naye sana. Nilimuhamisha tena shule ili tu awe huru, na hapo ndiyo alisoma nje.
Niliona amebadilika mwanangu, hata kama alipenda privacy lakini niliona utulivu wake sana. Alikuwa na akili vizuri kabisa mpaka anahitimu chuo. Amepitia mengi, anapambana kuwa Bora sana.
Niamini mwanangu usiniache peke yangu nimfundishe binti yangu thamani yake. Ameharibika kiakili na kuona anaweza kufanya anachotaka na kupata anachotaka yeye. Nisaidie kumfanya aamini kwenye upendo, nisaidie kumfanya ajue thamani yake.
Kuhusu kupenda najua anakupenda sana. Haitakuwa ngumu kwako tafadhali. Hadithi hii ni ndefu Ila kwa kifupi nimekuelezea ili kujua tatizo nini. Hata wewe unajua ni msichana mzuri, ni binti mzuri, mwenye upendo, huruma, mchangamfu.
Ni makosa yangu mwanangu, na nipo tayari kufanya lolote ili kumpa hii furaha ya ndoa binti yangu. Nakuomba mwanangu, nakuomba sana tumsaidie pamoja, usimuache atateseka sana anaumia, napambana asiwe kama mimi nilivyo fanya zamani hizo.
Tafadhali sana, sikuwa najua kuwa tabia mbaya za mzazi zinaambukizwa kwa mtoto haraka sana. Ndivyo ilikuwa nisamehe mwanangu nakutesa na makosa yangu, nisamehe kijana wangu, naomba, naomba sana tafadhali nakuomba nisaidie kumfanya mwanangu awe na furaha.
Hata mimi niliipa nafasi ndoa yangu, nikaachilia yote, nikawa mke kwa mume wangu, ingawa hajui mengi kuhusu kinachomtokea binti yake lakini ni baba mzuri sana, anatupenda sisi wote.