
LOML | Love Of My Life (112)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:112
Unaweza mwanangu, unaweza kuipa ndoa hii nafasi nyingine muhimu mfungue moyo na kuanza upya. Tazama mimi na baba yenu ni mfano mzuri kabisa, tuna furaha sana.β
Huyu mama alilia kwa uchungu nisimuache binti yake hata alipiga magoti na kushika miguu yangu. Nilimtazama kwa huruma sana na kumuinua nikisema βmama unafanya nini tafadhali keti.β
Huyu mama alilia sana, nilikuwa namtazama huku ndani ya moyo wangu naishangaa hii dunia. Ina mambo mengi ya ajabu mpaka kushangaa ni kazi ngumu. Kusema ukweli dunia ni ngumu sana.
Maneno aliyoyaongea huyu mama, haswa ni malezi yaliniuma sana moyo wangu, kumtazama nilijisikia aibu, aliamua kuniambia mambo magumu sana.
Nilijikuta nainuka taratibu huku huyu mama ananiita huku analia βMwanangu!!, mwanangu!!, tafadhali, mwenzako amekiri makosa yake, anaomba sana msamaha nakuomba.β
Niliendelea kutembea tu, nilitembea huku mazungumzo ya Yule mama yakijurudia nikiona namna gani wanawake wanatakiwa kulinda watoto wao.
Nilijisikia vibaya lakini bado sioni sababu ya binti huyu kunifanyia mimi haya kwasababu mimi sipo kama baba yake alivyokuwa kwa mama yake.
Niliamua kuishi naye kama mke hata kama nilikuwa natilia shaka upendo wangu lakini nilikuwa pale na yeye na wala sikumsaliti kama baba yake alivyokuwa akimfanyia mama yake.
Hata sikurudi tena ndani, mimi nilichukua usafiri na kuelekea hospitali ambayo mimi na familia yangu tunatibiwa, maana huku ni hospitali tofauti na ile.
Nilikuwa na hasΔ±ra sana, hasira sana kwasababu ya yote yaliyotokea haswa ile siku na mimba ya Gabriella kufanywa mpumbavu mbele ya mwanaume Kama Yule dokta mpumbavu.
Mimi nilifika mpaka hospitali, na sikujali wala kufuata utaratibu wowote nilipitiliza moja kwa moja mpaka chumba cha daktari. Alikuwa ana andika sijui vitu gani. Aliponiona alishtuka, Nilitabasamu na kumuuliza βunashtuka hukunitarajia au kwasababu unajua unachofanya na Gabriella.β