
LOML | Love Of My Life (113)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:113
Alianza kutetemeka, nilimkunja na kusema βwewe ni mshenzi sana, wewe ni muwakilishi wa madokta wote ambao wanatumia nafasi zao vibaya. Sitajali kama nimewahi kukuheshimu, sitajali kama umewahi kuwa rafiki kwa familia hata mimi.
Nakuahidi hutokalia hicho kiti na hakuna kitu utanifanya. Nitamwambia boss wako ushenzi wako wote na wake za watu, wagonjwa wanaokuja hapa. Nyie ndiyo mnachangia sana ukosefu wa amani kwenye maisha ya watu. Kwanini ulitembea na mke wangu eenh, kwanini?β
Dokta alikuwa analia akisema βnisamehe sana kaka, nakuomba tuzungumze nakuomba sana.β
Nilijikuta natetemeka, hapa Pina nilisahau kabisa ushauri wake, nilimpa kofi huku na kule, jamaa aliendelea kuhofu kuhusu kazΔ± tu akisema βNina familia kaka inategemea hii kazi tafadhali nisamehe sana.β
Nilimtazama na kutazama mikono yangu nikisema βwewe huna hadhi ya kuwa dokta, una roho mbaya sana, una roho mbaya.β
Nilibadilika mpaka uso, nikawa nakuwa mwekundu na natokwa sana jasho. Nilitokwa machozi ya hasira, niliona hapa naweza kufanya kitu kibaya. Na wakati huo simu yangu inaita sana. Nilijikuta namwambia kwa hasΔ±ra βutaona!!, Subiri utaona!! LazΔ±ma mkubwa wako ajue namna unaharibu biashara yake.β
Dr alikuwa analia hata ananipigia magoti, mimi nikiwa na hasira nilitoka. Nikatembea mpaka nje ya hospitali ka kutafuta usafiri mpaka ofisini kwangu huku muda mwingi simu inaita. Nilifika ofisini, nikaletewa funguo za simu yangu nikiambiwa Willy aliacha. Nikatazama ile simu ilikuwa ni mke wangu anapiga sana.
Sikutaka hata kupokea simu yangu, niliweka pembeni huku najiuliza βkwanini lakini nimeenda kumpiga Dokta, Sikutakiwa kufanya hivi. Ni kweli aliniona mpumbavu lakini nilipaswa kuachana na haya kama Pina alivyoniambia. Sikupaswa kumpiga Mungu wangu. Nisaidie, nisaidie na niongoze. Sitakiwi kuwa na hasira, sitakiwi kukasirika Kiwango hiki.β