
LOML | Love Of My Life (114)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:114
Nikiwa nawaza hayo, simu yangu iliita tena. Niliitazama ile simu, alikuwa ni mama yangu. Nilishusha pumzi na kujituliza kwanza halafu ndiyo nilipokea. Nilisema kWa upole βmama!!β
Mama alinijibu βupo wapi wewe jamani, kwanini unakuwa hivi mwanangu?β
Nilishusha pumzi na kusema βnisamehe sana mama, nisamehe sana nakuomba. Nilitakiwa nirudi kazΔ±ni haraka sana.β
Mama alisema βmwanangu, ni sawa vyovyote vile. Lakini wewe ndiyo ulipata wa kushinda hapa haijalishi ni namna Gani mmegombana eenh. Akishapona mtakaa mzungumze kuliko hivi inaonyesha picha mbaya kwa watu unakuwaje lakini.β
Nilishindwa hata kumjibu mama yangu, mama aliendelea βhaya mwenzako jioni hii anaruhusiwa, unatufuata au inakuaje?β
Nilijikuta nasema βmama sitaki kumuona huyo mwanamke kwasasa, nataka kuwa mwenyewe, tafadhali nielewe mama.β
Mama alishusha pumzi na kusema βMungu wangu wewe mtoto umekuaje?. Huyu ni mke wako mwanangu, ni mkeo huyu. Unatupa mtihani wazazi wako hapa unafikiri tutafanyaje. Hatuwezi kumuacha binti arudi kwao na mimi nipo. Mimi na baba yako tunaondoka naye, halafu utamfuata unanielewa?β
Nililalamika na kusema βmamaaa!!, mamaaaa!! , Gabriella ana kwao mama, ana mama muache mimi nishachoka, muache aendee.β
Mama alikasirika, Alikata simu na kisha nilibaki naita βmama!!, mama!!, hello mama!!β
Mama alikuwa tayari amekata simu, na mimi nilikuwa nataka tu Gabriella aende kwao na sio kwetu. Roho ilikuwa inaniuma sana. Nilikuwa naumia.