
LOML | Love Of My Life (115)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:115
Niliinamisha kichwa changu huku nakikukuna na kilikuwa hata hakiwashi, baba yangu alikuwa anapiga pia, nilitazama simu na kupokea. Baba alisema “mwanangu Rodricky, Nilidhani unanielewa kijana wangu.”
Nilishusha pumzi na kusema “baba kwasasa sipo tayari, sitamani kumuona.”
Baba alisikitika na kusema “maisha sio rahisi hivyo kijana wangu haswa kwenye ndoa. Sitaki kuzungumza sana kwasasa, kwasababu hata mama yake ana tia huruma sana.
Baba yake pia hili linamuumiza sana. Imebidi tu waseme watakaa na mtoto wao. Hii inatupa ügümü sana sisi familia yako na tunaonekana Kama tunaungana na wewe. Kijana wangu, nakuomba sana usiwe hivyo.”
Nilishusha pumzi yangu kwa nguvu, na kusema “baba!!”
Baba yangu aliniambia “sijui kuna kitu gani zaidi ya ulichoniambia. Lakini kusema ukweli mwanangu, mwenzio anajutia sana muda wote analia sana.”
Nilisema “baba!!”
Baba aliniambia “mimi na mama yako tunarudi nyumbani. Tutawasiliana wakati ujao.”
Niliita Tena “baba!!”
Baba yangu alikata tu simu.
Kwa mazingira haya, hata kazi ilikuwa ngumu sana kwangu. Nilikuwa nawaza mengi haswa kuhusu mambo mama yake mke wangu ameniambia. Mama mkwe wangu alikuwa anaumia sana, alikuwa analia sana.
Nilijisikia vibaya sana, lakini kama hivi ndivyo mbona mimi nampenda tu kwanini asitulie. Maskini dunia hii Ina mambo mengi sana ya maumivu. Maisha haya ni magumu sana. Watu wanapitia mambo mengi sana, watu wana trauma ambazo wanazificha na zinawaua kila siku.
Nilijikuta machozi yananitoka sana, malezi ya watoto ni muhimu sana. Kama mtu ameanza mapenzi umri mdogo namna hiyo. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kumfahamu mtu unayemuoa au kukuoa.

