SEASON 3: LOML | Love Of My Life (117)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:117
Nilisoma, nilisoma kwa kumuhurumia lakini Sikutaka kumzingatia, Mara uliingia mwingine “nipo nyumbani mume wangu, usinitelekeze kama hunijui. Naomba tuzungumze mume wangu. Nakuomba uje kunichukua.”

Nilisoma tu na kuona nachanganyikiwa. Niliamua kumpigia simu rafiki yangu Willy. Willy alipokea simu yangu na kusema “kaka Upo wapi?”
Nilimwambia kwa upole “Upo wapi?, leo nataka kunywa kidogo.”

Willy alicheka mna Kisha aliniuliza “kwema?”
Nilimwambia kwa kusema “hata sielewi kabisa, nataka tuonane tu nipunguze mawazo.”
Willy aliniambia “nakufuata hapo sio muda. Jiandae.”

Nilivuta pumzi na kusema “fanya haraka.”
Akaniambia kwa upole “naacha garı nakuja na pikipiki.”
Nilimtazama na kusema “ni sawa, Hakuna shida.”

Nilitoka nje mpaka kwa gari yangu, nilikaa nimejiinamia tu. Kiukweli sina raha kabisa, maisha yangu yote naona Hakuna raha naipata. Nilisubiri kwa muda, na Kisha rafiki yangu alifika.

Nilimfungulia mlango wa gari na akaingia, aliponiona tu, nilijikuta machozi yananitoka sana. Alinikumbatia kwa nguvu, akinipigapiga mgongoni na mimi nikiongea kwa uchungu “najikaza kaka nashindwa nashindwa kabisa.”

Willy alinituliza sana, Kisha aliondoa gari. Alinipeleka mpaka ufukweni. Nakumbuka sana. Tulishuka na hata nikamuuliza “umenileta hapa kufanya nini kaka?, nataka kulewa.”

Alinitazama na kuniambia “wewe ni ndugu yangu, siwezi kukupeleka kulewa kama sehemu ya küpünguza maumivu yako. Kaa hapa, Ila unavyotaka ukimaliza nakuomba niambie nini kinasumbua.”

Nilimtazama na kusema kwa upole “mke wangu kaka, mke wangu.”
Willy alishangaa na kuniuliza “mke wako?, mbona mlikuwa na furaha sana leo pale ndani.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata