
LOML | Love Of My Life (119)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:119
Kaka nisikilize, ukiwa karibu na Mungu wewe na familia yako na yeye atakuwa karibu nanyi. Trust me ninachokueleza No prayer goes in Vain(Hakuna maombi huenda bure) kila ukiomba Mungu anafanya namna. Nakuomba Kaka.β
Nilimtazama tu, na wakati huo simu yangu ilikuwa inaita. Nilipo tazama alikuwa ni baba yangu. Nilishusha pumzi, na kusema βbaba tena.β
Willy aliniambia βpokea kaka pengine kuna tatizo.β
Nilipokea simu ya baba yangu, nilipoitq tu βbaba!!β
Baba yangu aliniuliza βupo wapi?β
Nilimwambia kwa upole βnipo na rafiki yangu baba, kuna tatizo?β
Baba aliniambia βTatizo lipo, mkeo ametaka kujiua huko kwao, na unatafutwa hupatikani hivi kijana wangu una shida gani?β
Nilishtuka na kusema βbaba unasemaje?, kujiua kivipi, una maana gani?β
Baba yangu aliniambia βalikunywa vidonge vingi kwa wakati mmoja, muda huu ninavyo zungumza tupo hospitali. Fanya haraka Njoo hapa.β
Nilichoka, hata kutoa machozi mimi nilichoka. Nilipokata simu nilisema βGabriella alitaka kujiua wapo hospitali.β
Kaka Willy alishangaa na kusema βMungu wangu balaa gani hili, anaendeleaje?β
Nilimtazama kaka Willy nikisema βsijui hata nilikosa wapi, baba anasema wanaendelea vizuri Ila wapo hospitali.β
Willy alinitazama na kusema βtuondoke, fanya tuondoke.β
Safari hii hata kubisha sikuweza, niliingia ndani ya gari na kuondoka na safari ilikuwa ni kwenda hospitali. Nilipofika pale mama yake Gabriella aliponiona tu alilia kwa uchungu akisema βalitaka kufa mwanangu, alitaka kujiua. Tafadhali yamalizeni mwanangu nakuomba.β
Nilimtazama baba, na baba yake Gabriella walikuwa wamechoka wananitazama tu. Nilimkumbatia huyu mama ajisikie vizuri. Baada ya hapo niliuliza βmke wangu yupo wapi?β
Mama alisema βamepewa dawa ili apumzike. Sidhani kama unaweza kumuona.β