LOML | Love Of My Life (120)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:120
Wakati huo dokta ambaye sasa nimemfahamu alikuwa anapita. Niliita “doktaa!!, doktaaa!!, doktaaa!!”
Alisimama, na mimi nilimsogelea na kusema “tafadhali Naomba kumuona mke wangu.”

Dokta alisema “amepumzika utamuona kesho. “
Nilisema kwa upole “hapana kidogo tu Naomba kumuona,”
Dokta alinitazama na kusema “nifuate, dakika 5 tu.”
Nilimshukuru na kuongozana naye.

Alinifikisha mpaka chumbani, pale namuona mke wangu amelala tu. Nilimtazama na kujikuta naanza kucheka, nilikuwa nacheka huku naumia sana halafu nilisema “kwenye maisha yangu, sijawahi kuona mtu mbinafsi kama wewe. Wewe ni mbinafsi sana Gabriella. Kwahiyo ulitaka kujiua halafu mimi nionekane nimeua.

Wewe ni mbinafsi sana, Mara zote unafikiria kuhusu wewe tu, Mara zote unajiwaza mwenyewe. Una roho mbaya sana wewe, una roho mbaya. Kwanini unawaza kujiua. Badala ya kuwajibika na makosa yako unaya kimbia.

Uliwaza kuhusu mimi itakavyo kuwa, vipi kuhusu mama yako na baba yako namna wangeniona muuaji wa binti Yao kipenzi. Nimekukosea nini, Gabriella niambie nilipo kukosea kwanini ulikuja kwa maisha yangu na unanitesa namna hii.”

Nilijikuta napiga magoti nalia, kusema ukweli nililia sana, wakati nikiwa pale Giana aliingia. Alipo nikutane pale nalia namna ile, aliniinua kwa upendo akisema “shemeji tafadhali usilie, usilie shemeji yangu mambo yatakaa sawa.”

Nililia nikisema “kwanini ajiue, kwanini anataka mimi ndiyo nionekane na makosa, kwanini anakimbia makosa yake badala ya kuyakabili. Ni mbinafsi sana, ni mbinafsi.”

Giana alinikumbatia akisema “anatuhutaji sana, tafadhali shem msamehe na muanze upya. Hakuna mahusiano au ndoa Hakuna changamoto.

Anzeni upya na mfurahie maisha yenu. Nakuomba sana shemeji yangu. Acha kulia, Acha kulia na ujikaze. Muombe Mungu akujalie nguvu ya kuhimili maumivu haya. Muombe Mungu akutengeneze.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata