LOML | Love Of My Life (123)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:123
Kitu pekee unaweza kufanya sasa hivi, ni kujisahaulisha kila kitu kwasababu Mipaka yako itawaudhi wote waliozoea kukutumia ovyo. Nakuambia hivi kwasababu nimewahi kuwa kwenye hali kama hii, hali ya maumivu sana.

Najua nimechanganya Ila ukikaa ukatulia utagundua kuwa nilikuwa sahihi. Usiku mwema Rodricky, tafadhali acha kulia na utafute namna ya kutatua tatizo lako na mke wako.”

Nilibaki namtazama tu machozi yananitoka. Nilikuwa naumia na maneno yake. Kwasababu binadamu ndiyo walivyo hawana huruma na unajisikiaje kabisa. Pina aliniambia maneno makali na akawa anaondoka zake. Niliita kwa huruma nikisema β€œPina!!, usiondoke Naomba nikupeleke.”

Pina alinigeukia Akatabasamu na kusema β€œnitafika, una mambo mengi ya kumuelezea Mungu wako. Uwe na usiku mwema.”

Aliondoka zake na kuniacha pale, nilimtazama mpaka anapotea kabisa pale getini kanisani halafu mimi nikageuka ana kuanza kuelekea ndani ya kanisa. Nilifika kanisani, nilienda kulala tu madhabahuni.

Sikuweza kusema neno lolote, Ila Mungu alikuwa anajua kile najisikia ndani yangu. Nililala pale chini huku nagugumia tu, nilikuwa naumia sana kusema kweli. Başı nililala hapa mpaka asubuhi. Simu yangu niliacha kwa gari, niliamshwa asubuhi na watu wa Misa za asubuhi.

Baada ya hapo ndipo na mimi nilisali pamoja nao na nilipo maliza safari ya kurudi nyumbani ilianza. Nilichoka sana. Nikamuomba mama Babuu aniandalie Supu nikiwa naoga maana Nina njaa sana. Mama babuu hakuwa mbishi.

Başı nilifika chumbani, nyumba imepoa sana Ila nilioga na Baada hapo nilitoka kwaajili ya kula. Nilipokuwa nakula, huku maneno ya Pina yakinisumbua sana kuchwani hata nikawa sijui cha kufanya, nilisikia hodi mlangoni, mama Babuu alienda kufungua.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? FULL

KIBOKO YANGU FULL

JOGGING MASTER FULL