
LOML | Love Of My Life (125)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:125
Nakupenda sana mume wangu, nimekosa sana, nimekukosea mno, najuta mbele ya Mungu, padri wangu na familia pamoja na wewe mume wangu.
Nilikuwa mjinga na mpumbavu, lakini sipo tayari kukupoteza kwasababu nakupenda sana na najua siwezi kupata mwanaume kama wewe nakuomba sana.”
Mama yangu alikuwa ananitazama akisema “msamehe mwanangu, analia sana Muoneee huruma anaumwa.”
Kıla mtu akawa ananitazama nimsamehe, baba yangu alitaka hata nipigia magoti, nilijikuta nalia na kumuinua mke wangu na kumkumbatia.
Wao waliona kama nimesamehe Ila kwangu ilikuwa Bora ipite tu maana nimechoka sana. Walifurahi sana, wakapiga makofi. Amani ilitawala, nilimwambia mke wangu “acha kulia nimesamehe tuanze upya Ila sitavumilia tena ujinga huu.”
Mke wangu alinitazama na kusema “nataka kuwa mke kwasasa hata kazı nitapumzika ili niwe karibu na wewe mume wangu.”
Watu walizidi kufurahia. Tulibarikiwa, tukasali, tukala na nyumba ikawa na vicheko mpaka ile jioni wanaondoka wakitupongeza.
Tulibaki wawili na mimi nikaenda chumbani sina hata raha. Mke wangu alinifuata na kupiga tena magoti na kusema “najua una hasıra na mimi, nakuelewa mume wangu Ila nipo tayari kuwa mke wako tafadhali nipokee.”
Nilimtazama na kumuuliza “Upo tayari kuzungumza na mtu wa tiba ya akili, mnasihi.”
Alinitazama na Kisha aliniuliza “kwanini unasema hivyo mume wangu?”
Nikamuuliza “ulipanga kuniambia lini kuhusu wewe na mama yako?”
Aliinamisha kichwa na küsema “nisamehe mume wangu.Sikutaka kukusumbua. Nipo tayari kufanya lolote niwe Bora.”
Nilimwambia “atakuwa anakuja hapa, Hakuna kwenda kazini. Hatutafanya lolote mpaka nijiridhishe tabia zako na Baada ya hapo nitatimiza ahadi yangu ya Paris ili tukaanze upya kabisa.”

