LOML | Love Of My Life (126)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:126
Alinikumbatia akisema kwa furaha β€œnipo tayari mume wangu. Nakupenda sana.”
Nilimkumbatia başı tu nitafanyaje. Na hapa ndiyo maisha yalianza.

Maisha yalikuwa sio mabaya kusema ukweli. Mke wangu alionesha mabadiliko makubwa sana. Alibadilisha mpaka line ya simu. Tulibaki wachache kwenye maisha yake mimi, familia na rafiki yake Giana.

Alikuwa ana hudhuria vizuri darasa. Hata kanisani tulienda pamoja Ila ni karibu na huku nyumbani. Sikuwa na furaha maana sio rahisi kusahau lakini nitafanyaje na Pina nilikuwa nikimpigia hapokei tena simu yangu na akipokea akijua ni mimi anakata hivyo niliacha tu kumtafuta nikiamini nitamfuata kwao tuzungumze au kanisani anapopenda kwenda.

Niliona mabadiliko kama vile mke wangu kufanya kazi za nyumbani, kunifulia, kutandika kitanda. Mke wangu wa kΔ±sasa sana hivyo mambo yake yalikuwa yamekaa kizungu sana.

Alikuwa anapendeza sana na mimi nilimpa kila kitu. Nilijikaza wiki mbili tu baadaye tulianza kushiriki tendo ingawa ile Imani sina Ila maisha yalisonga. Mke wangu alikuwa amebadilika sana.

Hata mazungumzo, kucheka na mimi, kunitunza zawadi na mitoko mingi sana. Nilikuwa nafurahia mabadiliko haya huku na mimi nikipambana sana na kazΔ± zangu. Mambo yalikuwa mazuri kwa upande wetu.

Wazazi walifurahia maisha yetu, kuna siku tuliwaalika nyumbani na mawazo ni mke wangu alitoa. Akawa ni mtu mwenye upendo sana.

Tulitembelea marafiki kama Giana, Willy na mambo Kama haya. Taratibu nilianza kusahau madhira yote na kuona na kukubali kuwa mke wangu amebadilika.

Başı miezi miwili iliisha sasa tupo ndani ya mwezi wa 6 wa ndoa yetu. Mahaba ni yamekolea. Kila kitu kaacha mke wangu, unajua hana hata Muda tena na simu. Başı hii siku ilikuwa alhamisi.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BINTI MDUNGUAJI FULL

LOML | Love Of My Life FULL

CHAGUO LA MOYO FULL