
LOML | Love Of My Life (130)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:130
Watu wengi wamezoea kuona wanaume ndiyo wana matukio. Lakini niamini mimi wapo wanawake wengi sana kama mke wangu, wengi sana na wamejaa na wanaume hawana sehemu wana hema.
Mimi sikuwa Kama mjinga kumpa nafasi mke wangu, sikuwa mjinga kusamehe hata pale ambapo niliona sitaweza sana. Nimezaliwa, nimelelewa na ninatii maneno ya watu wazima hata kama wao hawaoni koΕa la mke wangu.
Lakini ndani ya moyo wangu, Yale maombi yangu, kule kusali kwangu, Mungu amesikia, Mungu amenivusha.
Unajua hapa ninavyolia ndiyo najua kuwa Ina maana Mungu amenipitisha hapa mimi, ili nijifunze kuwa imara, ili niwe mfano kwa kufundisha wengine upande mwingine wa maisha, sio Hilo tu, nimepitia maisha haya ya ndoa ili niseme Yale ambayo wanaume wengine wanashindwa kusema ingawa ni wengi sana wanaacha wake zao kwasababu ya tabia mbaya Kama za mke wangu.
Mungu ameniacha nipitie haya ili iwe funzo kwa wengine wote wenye tabia kama Gabby. Gabby hanidai nilipofika hapa, ndoa yangu kati na yeye imeisha.
Wakati nilipogundua kanisaliti nilimpa nafasi ya kujitengeneza nikiwa na tahadhari kubwa Ila yeye aliona kama vile mimi Sina pa kwenda na yeye ni mwanamke bora sana na Mungu amejidhihirisha wazi ili mimi nione kuwa ananifanyia uongo mkubwa sana.
KΔ±la ninapozidi kutembea ndiyo naona utupu wao juu ya kitanda changu. Machozi yanazidi kunitoka. Nilikuwa naumia kupita kiasi, nilikuwa naumia sana.
Nilifika mpaka karibu na sebuleni, nilikuta huyu mama Babuu amesimama anatokwa machozi. Aliponiona nalia na yeye alikuwa analia.