
LOML | Love Of My Life (131)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:131
Alinikumbatia kwa nguvu na kusema βNilijua ipo siku utajua hili, mwanangu hustahili kabisa haya. Hustahili kabisa.β
Nililia kwa uchungu nikisema βulikuwa unafahamu hili?β
Mama Babuuu alisema akilia βNaona aibu kuendelea kufanya kazΔ± hapa na Gabby. Nimekuwa naye kwa miaka mingi, sipendezwi na tabia zake kabisa. Haswa wewe ulipokuja kwenye maisha yake.β
Nilimtazama na kusema βsasa ndiyo naanza kukuelewa Yale maneno yako, sikuelewa kabisa.β
Mama Babuuu alifuta machozi na kusema βamekutumia kwa faida zake, amekutupa na kuona hufai. Hakikisha unaoza, unanuka, akikusogelea akimbie sana. Badilika mwanangu, asiweze hata kukukaribia. Hakufai.β
Nililia, nililia sana kwa maumivu makali, ni Bora hata ile ya mwanamke na wanaume wale. Sasa hivi ninacho kiona ni hatari.
Tangu nimezaliwa sijawahi kuona mimi, ndiyo Mara ya kwanza naona, ndiyo Mara ya kwanza nimeshuhudia kutoka kwa mke wangu.
Nilifika mpaka nje huku nalia, unajua natembea kama vile sijui nimepoteza nini. Nimeishiwa nguvu, nimepoteza akili. Nipo tu hapa duniani.
Nilipoingia ndani ya garΔ± nilimpigia sana simu Pina, hakuwa anapokea, Niliendelea kumpigia lakini hakuwa anapokea.
Niliondoa gari, niliendesha gari huku nalia tena sio sauti ndogo, nilikuwa nalia sauti kubwa ya maumivu ndani ya gari na kufika mpaka kanisani.
Nilipofika kanisani, nilisimamisha gari tu nje ya kanisa. Haikuwa siku ya Ibada wala, lakini mimi niliingia kanisani. Pale katikati ndiyo Mimi nilipiga magoti, nililia sana. Nililia kwa maumivu makali.
Sikuwa na mtu wa kumwambia akanielewa zaidi ya Yesu pekee, nilikuwa ninateseka na haya maumivu mpaka ninachanganyikiwa.
Nilijikaza nikainuka, nikapepesuka mpaka kwenye kiti. Nilikumbuka Nina simu ya Gabby mfukoni. Nilichukua ile simu, na kufungua.