
LOML | Love Of My Life (137)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:137
Nilimtazama na kusema “sijaongea na dokta unajua, hata sielewi.”
Alitabasamu na kusema “pole sana, get well soon, Ricky.”
Niliposikia kizungu hivyo nilitabasamu lakini sasa kila mtu cha get well soon anajua. Nilimchokoza kidogo na kusema “thanks so very much Pina, thanks!!”
Alitabasamu na kunishika mkono wangu, aliniuliza “for What Ricky?”
Nilimshangaa na kumuuliza “unajua lugha hii?”
Alitabasamu kidogo na alisema “muone, watu wengi hufikiria watu maskini hatujasoma. Mimi nimesoma ingawa sio sana ila ninajua mengi kuhusu afya. Nilisoma diploma ya clinical Officer, nilifanya kazi kidogo na baadaye nikaacha.”
Nilishangaa nikisema “waooooo!!, waooooo!! Kumbe nipo na dokta hapa.”
Alicheka kidogo akisema “acha kelele mgonjwa.”
Nilitabasamu na wakati huo Willy alikuwa anaingia. Willy alisema “umepona sasa hata sauti inatoka, au Pina ana dawa tofauti.”
Nilitamani kucheka ila sikuwa naweza, nilitabasamu nikitazama Pina anachela na kusema “na bora umesema ukweli maana ungenidanganya?”
Willy alicheka na kusema “mimi ni msema kweli. Sasa naomba sogea kidogo nimlishe.”
Pina alitabasamu na kusema “naomba niandalie vizuri, nitakusaidia kwakuwa mimi nipo.”
Willy alishangaa, kisha Pina alisema “naweza, hakuna kitu siwezi kufanya. Naomba.”
Basi Willy aliandaa Supu, na kisha mimi alinikalisha vizuri na kisha nilianza kunyweshwa Supu.
Usawa uleule alianzia mwanzo wakati anatafuta mdomo wanngu ndiyo alinipa. Alinilisha kwa upendo sana, nilikuwa natabasamu tu, hata Willy alikuwa anaona hilo. Nilikuwa nafurahia kulishwa na Pina sana.

