LOML | Love Of My Life (140)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:140
Pina alitabasamu na kusema β€œhiyo nasali kΔ±la Mara, sipendi kumfokea Mungu kabisa. Kwasababu najua ananipenda.”

Nilitabasamu na kufunga macho yangu nikisema β€œMungu kama nimewahi kukufokea kwenye maombi yangu, nisamehe sikumaanisha.”

Nilifungua macho yangu na kukuta Pina anatabasamu. Kisha Baada ya hapo alinishika mikono yangu na β€œMungu baba yangu wa Mbinguni, umenibariki kwa namna nyingi sana na nakushukuru sana.Ninatambua mipango yako juu ya maisha yangu ni mikubwa na inapita uelewa wangu.

Naomba uniongoze na uzidishe imani yangu kwako baba yangu.Ninaweka maisha yangu, Δ°mani yangu, kazi yangu, namuweka Ricky, na kesho yangu nisiyo ijua mikononi mwako.

Ulinivusha na Yale, ninakuamini sana kwenye haya, nina imani na wewe bila wasiwasi wala kusita.Ongoza maisha yangu na wote walio nizunguka.

Adui zangu wasiniweze wala kunisogelea, nifanye wapekee na vile unavyotaka. Watu wakiniona mimi wakuone wewe Mungu wangu. Wewe ni kimbilio langu siku zote za maisha yangu.

Kitu pekee sijutii kwenye maisha yangu ni kukufahamu wewe, Nakupenda sana Mungu wangu wa mbinguni.Nakupenda.”
Nilitabasamu na kumuuliza β€œninaweza kurudia na mimi, na Kama nikikosea utaniongoza.”

Pina alitabasamu na kusema β€œbila Shaka, tunaweza pamoja.”
Başı kwa pamoja tulianza ingawa nilikuwa Nachanganya na kukosea sikuacha kumpa nafasi Pina ya kuniweka sawa kwenye Hilo. Nakumbuka sana ulikuwa wakati mzuri sana.

Pina alinitazama na kusema β€œnilikuwa naogopa sana, niliogopa kukupoteza sijui kwanini nilipata hofu hiyo.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata