LOML | Love Of My Life (141)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:141
Nilimtazama na kusema kwa upole na maumivu β€œPina najuta kwanini sikukusikiliza ile siku pale. Maisha yangu yamekuwa ya kutisha sana. Ulikuwa sahihi sana, na kosa langu lilikuwa ni kumsamehe tena na tena. Nilikuwa mjinga sana, nilikuwa sio mtu wa kujielewa kabisa. Mimi ni mpumbavu.”

Pina alitabasamu, akanifuta machozi ambayo yalikuwa yanatoka β€œhapana wewe sio mjinga, wewe sio mpumbavu Ricky. Wewe ni mtu mzuri sana, wewe una moyo mzuri sana na ndiyo maana unajua kusamehe kwasababu unajua kuhusu upendo.

Hujapoteza kitu, yeye ndiye amepoteza. Wewe ni kati ya wanaume wachache ambao kΔ±la mwanamke anatamani kuwa naye. Wewe ni Bora sana.”

Nilimtazama Pina na kusema β€œkuna watu kweli kabisa hawahitaji nafasi ya pili. Pina nawaza hivi kuna wanaume wameoa matatizo namna gani?. Watu wengi wanaigiza wema, hekima na furaha ya wongo mbele ya watu kumbe hawana maana kabisa.”

Pina alinishangaa na kuniuliza β€œIna maana Gani Ricky?”
Nilimtazama Pina, yeye pekee ndiyo huwa naweza kuzungumza naye.

Nilijikuta nafunga macho yangu, machozi yananitoka na kusema β€œMke wangu, ana mahusiano na mwanamke mwingine ambaye ni rafiki yake kipenzi. Mwanamke mwenye hekima sana Kumbe hana lolote.”
Pina aliniambia kwa upole β€œsijaelewa, unaweza kurudia tena?”

Nilishusha pumzi nikilia na kusema β€œsijamkosea Pina, ni kweli kwa macho yangu nimewakuta wanafanya mapenzi.”
Pina alijiziba mdomo, machozi yakatoka na kusema β€œMungu wanguuuuu!!!”

Nililia nikisema β€œnajiona sina maana, sina nguvu, nimechanganyikiwa kabisa mimi.”
Pina alisema kwa upole β€œsijui hata ni kiti gani hiki. Pole sana Ricky. Hii ni ajabu kwa Mara ya kwanza nimejisikia kuchoka sana.

Upo sahihi kuhimili hili ni ngumu. Kivipi sasa, dunia Ina enda wapi hii Mungu wangu. Pole sana Ricky. Mara zote kumbuka Wema ukizidi unakaribisha dharau. Ndiyo kama hizi.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UKO HOME NIJE FULL

BIOLOGY TEACHER FULL