
LOML | Love Of My Life (149)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:149
Nikawa nawaza nimjibu nini bibi yangu, lakini kama bahati hivi mlango uligongwa. Kushtuka na kwenda kufunga alikuwa ni mtoto wa jirani anaomba beseni La kufulia.
Nilikaa kitandani nawaza sana naona kama ndoto zina maana na napuuza, wakati nawaza bibi yangu alinipigia.
Haraka nilipokea na bibi yangu aliniambia kwa upole โhujambo mjukuu wangu, una muda lini nataka kuzungumza na wewe.โ
Nikamuuliza bibi yangu โkwema bibi yangu?โ
Bibi aliniambia kwa upole โkwema kabisa na mbona hujaenda kanisani.โ
Nikamjibu bibi kwa upole โnilichoka sana bibi, nisamehe tu. Najiandaa hapa nakuja sio muda unahitaji chochote?โ
Bibi yangu aliniambia โnakuhitaji wewe mjukuu wangu.โ
Nilicheka tu ila ndani ya moyo wangu nilipata hofu.
Nakumbuka nilikata simu Baada ya hapo Mimi nilijiandaa Kisha nilipita sokoni ndivyo nilivyo nikiwa naenda kwa bibi yangu au mtu wa karibu najua nitashinda huko basi nikanunua nyama, viungo na vitu vidogo vidogo nilivyo na uwezo navyo nikaenda mpaka kwa bibi yangu.
Niliwasiliana na mpenzi wangu na kumuelezea juu ya safari yangu na alikuwa pamoja na mimi.
Baลฤฑ nilifika kwa bibi, tulipika, tulikula pamoja na tulipomaliza bibi yangu aliniambia โmjukuu wangu usiku nimeota ndoto hata sielewi.โ
Nilimtazama na kuuliza โndoto Gani bibi?โ
Bibi yangu aliniambia โnimeota unaolewa na Isack lakini gauni yako ya harusi ni fupiii sana, fupi hata huwezi kwenda kanisani wakati tulikuwa nayo ndefu tukawa tunajiuliza hata imekuaje.โ
Nilishangaa na kusema โunajua bibi lazฤฑma kuna kitu, hata mimi nimeota Mara shela jeusi, Mara shela limechakaa hata sijui ni kwanini. Nimeanza kuogopa bibi.โ

