
LOML | Love Of My Life (152)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:152
Hadithi yetu ikasambaa sana unawaona wale, walifunga ndoa wakiwa peke yao hakuna hata ndugu waliofika sijui hawana wazazi.
Ilikuwa inaumiza mno. Nakumbuka hata picha hami ya kwenda kupiga iliishia kanisani. Baada ya kurudi nyumbani kwa mume wangu alilia sana, alilia kwanini familia yake inamkosea namna ile.
Alilia akisema βwananifanyia nini sasa mbona mimi najitoa kwa mambo yao eenh, mbona Mimi nawapenda sana kwani kosa langu ni nini?β
Nilimwambia mume wangu kwa upole βmpenzi tafuta muda uongee nao ili kama kuna tatizo tutatue mapema kuliko namna hii.β
Mume wangu aliumia sana, ilikuwa ni siku ya furaha lakini tulimaliza kwa hΓΌzΓΌni sana. kwasababu mimi na mpenzi wangu tunapendana baΕΔ± kΔ±la kitu kilikuwa kinaenda sawa tulikuwa tunajitahidi kuficha maumivu yetu.
Kazini nilipewa Muda wa mapumziko kidogo. Hivyo nilitumia siku hizi na mpenzi wangu. Ni wazi mume wangu alizingumza na familia yake kwa maana mama yake alipiga simu siku hii. Na alitukaribisha nyumbani kwaajili ya mazungumzo.
Mimi niliogopa sana kwasababu nilipoenda awali sikupokelewa vizuri. BaΕΔ± mume wangu aliniambia βmke wangu nataka kutengeneza kati yako na mama yangu, tafadhali Naomba twende huna sababu ya kukataa.β
Kwasababu ya heshima yangu kwa mume wangu basi nilikubali. Kesho yake tulijiandaa na tulienda. Tulifika mpaka hapo nyumbani, tulikuta familia ikiwa pale. BaΕΔ± mama alipotuona tu alisema βeenh mwanangu mbona ushaanza kukonda mkwe wangu au hujui kupika nini?β
Tulicheka tu huku mume wangu akisema βmbona nipo vilevile tu mama. Mke wangu anajitahidi sana kuhakikisha nakula vizuri.β
Mimi nilitabasamu tu huku najua moyoni ni dongo lile. BaΕΔ± Tulikaa na mama ndiye alisema βnajua mmekasirika hatukuja kwa ndoa yenu. Tusameheni sana kwasababu kusema kweli sisi hatukujua una maanisha hivi umemzalisha Faraja na umekuja kuoa Pina kama familia hatukuwa na namna na wakati Faraja yupo na sisi miaka yote. Ila tutafanyaje na ushaamua. Farajaaaa!!, Farajaaaa!!, Faraja Njoo mwanangu.β