LOML | Love Of My Life (156)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:156
Nililala mpaka saa moja mtoto analia nasikia mdada anasema “wifiii!!, wifiii!! “
Nikamwambia kWa upole “ingia tafadhali.”
Aliingia, alikuwa mdada wa kazi. Alitabasamu na kusema “pole sana, mtoto analia sana.”

Nilitabasamu huku moyoni nalia na kusema “sana yaani. “
Huyu binti alisema “mama kasema ukiamka upike, na utumie jiko La mkaa. Naomba hela nikakununulie vitu vya kupika.”


Nilijisikia uchungu sana moyoni nililia sana. Sitamani kukumbuka hii siku. Hali ambayo nilikuwa nayo na sasa naambiwa tena nikapike tena kwa jiko La mkaa nililia sana hata huyu dada wa kazı alinitazama kwa huruma na kusema “nikusaidie mtoto?”

Nilimtazama na kusema nikilia “wewe nenda nakuja sasa hivi.”
Rodricky wacha niishie hapa leo, nina maumivu sana. Kwasababu siku hii ndiyo kama niliyafungulia maumivu ya maisha yangu. Kule kulia nililia, Yale maumivu, kwenye maisha yangu sitamani tena maumivu, simuhurumii mtu tena naona tu naishi dunia ya peke yangu.”

Nilimtazama na kusema “Pina!!, simulizi yako inasisimua sana natamani kujua ilikuaje na ikawaje hata upo hivi sasa. Lakini Pina nikuulize kitu?”

Pina alikuwa analia bado, nilimfuta machozi na kusema “Karibu Rodricky.”
Nilimfuta machozi, na kumtazama nikisema “Upo tayari kupenda tena?”

Alitabasamu na kusema “Nani atakaye taka kupendwa na mtu Kama Mimi, kipofu tayari nimeharibu maisha yangu.”
Nilimtazama na kusema “Vipi Kama yupo Pina.”

Pina alitabasamu na kusema “umechoka sasa Rodricky lala, nakuahidi kesho nitajitahidi nimalizie.”

Nilimshika mkono na kusema “Pina, mimi Rodricky tangu siku ya kwanza nimekuona. Nimekupenda sana. Nimejitahidi sana kuzuia hisia zangu na kuokoa ndoa yangu lakini moyo wangu unanirudisha kwako na nakupenda jinsi ulivyo kila siku ni zaidi ya jana. Nakupenda sana.”Pina alinishangaa na kuniuliza “Unanipenda mimi?, haiwezekani. Sitaki uteseke au uumie na mimi tena. Tafadhali usiniambie hivyo.”

Nilimshika mkono na kusema “Pina nimekuambia hivi ili ujue nakupenda. Just know that nakupenda sana. Sio kwasababu naumwa hapa. Mimi nakupenda wewe zaidi ya unavyo fikiria. Najua sasa sio wakati sahihi, lakini natamani kuwa pamoja na wewe. Wewe niumize,

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata