SEASON 4: LOML | Love Of My Life (159)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:159
Rodricky kamwe siwezi kukuacha peke yako, mimi ni mwanamke ninayejua thamani ya heshima na upendo. Nipo na wewe muda na wakati wote ukihitaji uwepo wangu.

Kwasababu, nakupenda sana Rodricky.Kwasababu nipo salama zaidi wewe ukiwepo kwenye maisha yangu. Acha hisia ziongee Kipenzi, nipo nje, ukihitaji lolote nitakuwa nasubiri.”

Hata mimi mwenyewe nilishangaa sana tena huku natabasamu, mimi sikuamini kama anaweza kufanya hivi tena mbele ya mama yangu na mwanamke mwingine ambaye anajifanya yeye ni kila kitu kwenye maisha ya wengine.

Natamani ungemuona Pina vile anatabasamu wakati mama kavimba, na Gabby ndiyo kama anataka kupasuka na wakati hafai hata kukasirika alipaswa hata asiwepo hapa.

Nilitabasamu, na alitembea mpaka mlangoni na kusimama, alisema β€œRicky Kipenzi, hata iweje usisahau namna unajisikia.”
Nilitabasamu, Willy anashangaa mpaka anataka kuanguka.

Alitoka nje na Pina. Wakati huo Gabby analia akisema β€œSio saawa Ricky.Kwanini unanifanyia hivi. Mimi bado mke wako. Tafadhali acha haya maigizo yako?”

Nilimtazama na kumuuliza kwa hasira β€œuna pata wapi nguvu ya kuzungumza haya tena kwa kulia kabisa. Au kwasababu ya ubaya wa dhambi yako unahisi naogopa kumwambia kila kitu ulichokitenda?.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL