
LOML | Love Of My Life (160)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:160
Umepata nguvu wapi ya kuja kusimama mbele yangu na kulia kama hakuna kitu kimetokea. Sijakufanya kitu kibaya, sijawahi kukuumiza kama nilivyo paswa kufanya.
Tangu awali nakuoa sikukupenda, kila mtu anajua hilo lakini nilipata nguvy ya kukupa nafasi kama mke nikakupenda na kukujali na ukafanya ninj Gabby.
Haya yote hakuna hata una stahili kwasababu wewe unatakiwa kuumia kama hutokuja kuumia tena. Pengine hujaelewa, maumivu yako hayanizuii kuishi, kufanya maisha mengine unajua kwanini, kwasababu maumivu yanayotoka kwa mwanamke ambaye hana akili hayadumu kwa mwanaume mwenye upendo na akili timamu.
Nakuchukia, nachukia siku ambayo ulikuja kwenye maisha yangu, nachukia kukuona, karibu na ndugu zangu wala mbele yangu. Sikupendi, sikupendi na ndoa yangu mimi na wewe sio kuisha Imekufa kabisa. Gabby hata kichaa hawezi kuwa na mke mshenzi kama wewe.β
Gabby alikuwa analia akisema βRicky pleaseee!!β
Huku mama akisema βinatosha!!, nini shida kwani ninyi watoto.Eenh Ricky nini kinaendelea. Kwanini maneno makali hivi kwa mkeo, kwani nyie watoto hamuwezi kuelewana hata kidogo kwanini?β
Nilimtazama Gabby na kusema βtokaaaaa!!, tokaaa!!, tokaaaaaaa!!, tokaaaaaaaaaaaaaa!!!β
Gabby alinitazama analia na kufungua mlango kuelekea nje huku mama akinituliza na kusema βunaumwa unajua, kwanini unafanya hivi lakinu eenh!!β
Mimi nilikuwa nalia kwa maumivu. Mama alinikumbatia na kuniambia βmwanangy tafadhali tulia, tulia tafadhali.β
Nilishusha pumzi nikisema βmama nahitaji kuwa mwenyewe nakuomba.β
Mama alinitazama na kusema βkivipi, umelala hapa siku mbili bila mama wala baba yako. Haitoshi wewe ni mume wa mtu mbele yangu una mwambia mwanamke mwingine una mpenda sana.