LOML | Love Of My Life (161)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:161
Tena mbele ya mama yako na mke wako hamna hata aibu na yeye alivyo kosa adabu anajiona anajua sana mapenzi. Umemtoa wapi yule maskini tena kipofu.

Mwanangu usiniambie kuwa unachanganyikiwa. Hamuendani, sio mwanamke wa aina yako. Naomba niambie sio kweli mwanangu. Kamwe huwezi kuwa na mwanamke wa namna ile.”

Nilijikuta namtazama mama nikisema β€œhivi mama mimi ni mwanao kweli kutoka kwenye hilo tumbo?”
Mama alinitazama na kuniuliza β€œunauliza nini sasa?”

Nilitabasamu na kusema β€œina sikitisha, mama kipenzi, hajui maumivu ya kijana wake wa kipekee tena kipenzi chake kama anavyosema. Mama yangu wewe hujawahi kujishughulisha na ninajisikiaje, inauma au haiumi.

Na sasa upo hapa unanipangia namna ya kupendana. Na sijui kwanini unapata nguvu ya kuita binadamu mwingine maskini, hatuendani na kipofu. Hivyo ndiyo sababu ya wewe kusali mama, kuita watu majina ya ajabu?.

Haya sawa tufanye ndiyo ulivyo, vipi kuhusu maumivu yangu na mwanamke wa hadhi yangu, tajiri, asiye kipofu mwenye macho yote. Natamani kila mtu angejua alichofanya lakini haiwezekani.

Siwezi kusema kwasasa, lakinu nakuambia tena hapa mama. Sitaki mtu yeyote, sitaki mtu mwingine yeyote aniambia kuhusu Gabby. Mimi na yeye tumemaliza. Ndoa yetu inekufa na haiwezi kufanikiwa tena.

Sijui kama Pina yeye amemaanisha, ila kiukweli natamani angeniambia maneno haya tena na tena na tena. Kwasababu ni mwanamke wa pekee sana kwangu, yupo na mimi, anajali na kuyajua na kuyaelewa maumivu yangu.

Mimi na yeye tunaongea lugha moja. Mama sitaki kumuona Gabby karibu na wewe wala baba yangu wala familua yangu. Nina chukia sana.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

UTAMU WA JAMILA FULL

BIOLOGY TEACHER FULL