
LOML | Love Of My Life (163)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:163
Mama alibeba mkoba wake kwa hasira na kutoka. Nilibaki nimekasirika sana. Nilikasirika kwa maneno ya mama yangu. Alivyo zungumza kuhusu Pina, na namna anataka mambo yawe.
Lakini baada ya kukumbuka maneno ya Pina. Busu lake nilitabasamu. Na wakati huo dokta alikuwa anaingia. Niliendelea kutabasamu hata akasema βnaona una furaha sana.β
Nilitabasamu na kusema βmaisha yananipa sababu ya kutabasamu kwa mara nyingine.β
Dokta alitabasamu na kisha aliendelea na kazi yake na kusema βulikuwa unaendelea vizuri, kwasasa naona hali yako imebadilika tena. Sikia nikuambie kitu Rodricky, unatakiwa kutulia kabisa ili hali hii ikae sawa usifanye masihara tafadhali sio nzuri.β
Nilivuta pumzi na kusema βnimekuelewa tafadhali, nitakuwa makini. Naomba ukitoka hapo niitie Pina na Willy.β
Dokta alinitazama na kusema βPina sijamuona. Willy yupo.β
Nilishtuka, huku moyoni nikijiuliza βina maana ameondoka?β
Nilitamani kujua hili kutoka kwa Willy. Dokta alimaliza mambo yake na kisha alitoka. Alipotoka tu haukupita muda sana Willy aliingia ana tabasamu. Sikuacha hata amalize kutabasamu nikamuuliza βKaka Pina ameondoka?β
Willy alinitazama na kusema βkaka kile chuma umetoa wapi?β
Nilimtazama na kusema βuna maana gani?β
Aliniambia βniahidi utanisimulia kila kitu kuhusu yeye. Sio poa, amenyooka hivi, haogopi na hapo ni haoni lakini Mungu wangu!!, Mungu wangu!!!β
Nikamuuliza Willy βacha mafumbo, niambie nini kimetokea?β
Alishusha pumzi na kusema βbaada ya kutoka hapa, alionekana hana raha hata nikamuuliza kama yupo sawa. Alinijibu tu nisijali yupo sawa.
Baada ya muda mkeo alitoka analia, na moja kwa moja alikuja mpaka kwa Pina. Sasa si unajua Pina haoni, mkeo alianza kupiga kelele zake na tambo nyingi akimtaka Pina akae mbali na wewe.