LOML | Love Of My Life (164)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:164
Pina alinyamaza tu, alipokosea mkeo alianza kusema mwanamke mshamba kama wewe, ndiyo maana umenyimwa macho hakuna mwanaume atakaye kutaka huna hadhi wala heshima unanichefua.”

Nilishangaa Pina amesimama ameanza kucheka, oya mwanangu nikaona hutakiwi kupitwa. Nikatoa simu na kuanza kuwachukua video bila wao kujua. Pina chuma ndugu yangu, unajua amemwambia nini?, shika simu uone ilivyokuwa ingawa sio ndefu sana maama huko mbele walianza pigana ikabidi nisaidie.

Nilikuwa napokea simu na kisha niliona Gabby bila aibu anavyotamba kwa kujiona ni bora sana, sasa upande wake alikuwa anamalizia na Pina sasa ndiyo anacheka. Kwanza anavyocheka sasa.

Uzuri wake unazidi na kisha alisema β€œhongera sana, umefanikiwa kwa mengi kwa urahisi sana. Wewe ni kweli mzuri, uzuri wako unakusaidia kitu gani. Ni kweli una macho lakini macho yako yameshindwa kuona uzuri wa mwanaume anayekupenda kwa dhati. Nisikilize.

Umetimiza ndoto zako kirahisi sana, kwasababu wewe umezaliwa kwenye familia nzuri na bora sana, familia ambayo ulipewa 5 ukaongezea 5 ukapata kumi, au ulipewa 7 ukaongeza 3 kupata 10, Pengine ukapewa 9 ukaongezea 1 kupata 10 au pengine ile 6 wewe ukaongezea 4 tu ukapata zako 10.

Hujafanya chochote kwasababu hata hicho ulichokuwa unaongezea kilitokea hapohapo, wewe ulichofanya ni kuongezea tu. Hii wala isikufanye ukajiona bora, ukadharau wengine, ukaona ni zaidi ya wale tuliotoka familia ambazo hazikuwa na chochote kile.

Labda nikukumbushe hata 0+10 bado jibu ni kama lako kumi. Sasa huwezi kushindana na mtu ambaye familia yangu ilinipa sifuri nikapambana kutafuta 10 ili niweze kuwa hivi nilivyo.

Tupo tofauti si unaona, hatufanani si unaona, wewe huwezi kuwa mimi, na wala mimi kamwe siwezi kuwa wewe.Busara ni wewe kuheshimu kila mtu anaye pumua na kuzichanga karata zake vizuri ili maisha yake yaende.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIBOKO YANGU FULL

TOBO LA PANYA FULL

UKO HOME NIJE FULL

JOGGING MASTER FULL