
LOML | Love Of My Life (166)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:166
Atakuwa ana maanisha?. Amesema atamuonesha namna natakiwa kupendwa na kuheshimika. Maneno yake kaka, yupo wapi kwani?β
Willy alivuta pumzi na kusema βbaada ya kumshika shemeji atoke nje, alikuwa anasema sitakubali hili, nitakuonesha hiyo 10 inakuaje, wewe si unajiona kichaa, siwezi kuacha unamchezea mume wangu, nitakuonesha.β
Wakati huo na mama yako alikuwa anatoka, alimfikia Pina na kumvuta bila hata kutaka maelezo nikawafuata nyuma. Walisimama nje ya hospitali na sijui wanaongea nini.
Nilimwambia Willy βnamfahamu mama yangu, naomba umfuate tafadhali mwambie namuhitaji.β
Willy alinitazama na kusema βhalafu utaniambia?β
Nilitabasamu na kusema βkila kitu, niitie kwanza.β
Nilitabasamu tu na Willy alitabasamu. Alikaa huko kwa muda huko aliponfuata wakati huo mimi nikikumbuka sakata la Pina na Gabby nacheka, Pina ni jasiri sana nilijikuta natabasamu, na vile vibao ndiyo kabisa na kisha akarudi akiwa peke yake.
Nikamuuliza kwa kumshangaa βVipi mbona peke yako?β
Alinitazama na kusema βamenipenda mwenyewe, amenifuata mwenyewe tatizo sio mimi hapa, tatizo ni kijana wako. Ongea naye mwambie aniache akiweza nitamuacha kama hawezi mama itabidi unipokee kama binti yako kipofu hapo vipi mama.β
Nikamtazama Willy na kusema βndiyo nini?β
Willy alisema βndiyo Pina amemwambia mama yako hivyo?β
Nilijikuta nacheka nikisema βeenh Bwana eenh?β
Willy alisema βusicheke, anaumia, yupo nje hapo analia, anajikaza tu lakini wanamwambia maneno mabaya sana.β
Nilijikuta najisikia vibaya na kusema βnaomba niitie tafadhali, nahitaji kuzungumza naye.β
Kabla Willy hajaamka, Pina aliingia na kusema βnipo hapa Rodricky.β