
LOML | Love Of My Life (168)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:168
Pina alisema βnooo!! Nooo!!, noo!! Ulifanya kitu hata Mungu anapenda tufanye. Ulisamehe na kuendelea na maisha. Yule mwanamke ndiyo mjinga sana, yeye ndiyo kipofu haoni, kabisa yaani alishindwa kupokea nafasi ulizompatia.β
Nilitabasamu na kusema βuwepo wako pembeni yangu ni zaidi ya kila kitu Pina. Wewe ni mwanamke ambaye unanifanya nijisikie vizuri sana ndani ya moyo wangu. Unanipa sababu ya kuwa imara, unanijali sana na kunipenda.
Wewe ni zadii ya bahati kwangu. Pina wewe ni Hatima yangu you are my Fate, my fortune and my smiley, ninakupenda haki ya Mungu. Sitamani kukupoteza. Nitafanya kila kitu uwe na mimi, ubaki hapa na mimi.
Tafadhali niambie, unanipenda?, sahau kuhusu maumivu, kila kitu kwasababu mimi sijali chochote ninachojali ni kitu kimoja tu unanipenda?β
Pina aliniuliza βhuogopi kuumia wakati bado una maumivu?β
Nilimtazama na kusema βkama yanatoka kwako sijali, sijali kwasababu yatatoka kwa mtu ninaye mpenda sana.β
Pina alitabasamu na kusema βWilly huyo amekuambia kuhusu Fortune, smiley na fate eenh.β
Nilitabasamu na kisha alinigeukia, akaniambia kwa upole βtangu siku ya kwanza nimekuona kanisani, nilijua hili litatokea. Nilipo sikia sauti yako, ndani ya moyo wangu nilijihisi tofauti sana.
Nilifanya juhudi za kukaa mbali na wewe lakini hisia zimeshindwa kabisa. Kelele za nakupenda, nakupenda, nakupenda zilikuwa ni nyingi ila ningefanya nini na wewe ni mume wa mtu Ricky.